Ansarullah Yemen yasema iko tayari kusaidia taifa na muqawama wa Palestina
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i98878-ansarullah_yemen_yasema_iko_tayari_kusaidia_taifa_na_muqawama_wa_palestina
Katibu Mkuu wa harakati ya Ansarullah ya Yemen ametangaza utayarifu wa Sana'a kulisaidia taifa na mapambano ya ukombozi wa Palestina katika kikao chake na mwakilishi wa harakati ya Jihad ya Kiislamu ya Palestina.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 17, 2023 04:00 UTC
  • Ansarullah Yemen yasema iko tayari kusaidia taifa na muqawama wa Palestina

Katibu Mkuu wa harakati ya Ansarullah ya Yemen ametangaza utayarifu wa Sana'a kulisaidia taifa na mapambano ya ukombozi wa Palestina katika kikao chake na mwakilishi wa harakati ya Jihad ya Kiislamu ya Palestina.

Kwa mujibu wa tovuti ya Al-Masira, akizungumza na mwakilishi wa Jihad Islami mjini San'aa Ahmad Barakah, Abdul Malik Badr al-Din al-Houthi, Katibu Mkuu wa harakati ya Ansarullah ya Yemen, amesisitiza msimamo thabiti na imara ya Yemen katika kuliunga mkono taifa la Palestina dhidi ya adui Mzayuni.

Katibu Mkuu wa Ansarullah pia amepongeza misimamo ya kishujaa ya wapiganaji wa harakati za ukombozi wa Palestina hususan harakati ya Jihad ya Kiislamu katika vita vya kulipiza kisasi cha uhalifu wa Israel.

Kwa upande wake mwakilishi wa harakati ya Jihad Islami nchini Yemen ameshukuru uungaji mkono wa kijasiri wa taifa na kiongozi wa mapinduzi ya Yemen kwa taifa la Palestina.

Ikumbukwe kuwa, mara kwa mara watu wa miji tofauti ya Yemen wamekuwa wakiandamana na kutangaza uungaji mkono wao kwa mapambano ya watu wanaodhulumiwa wa Palestina.