Jun 27, 2016 16:08 UTC
  • Erdogan apiga magoti na kumuomba radhi Putin

Rais wa Uturuki amemwandikia barua mwenzake wa Russia, Vladimir Putin akimuomba radhi kutokana na kuangushwa ndege ya nchi hiyo katika mpaka wa Uturuki na Syria.

Ikulu ya Rais wa Russia Kremlin imetoa taarifa ikisema kuwa, Rais Recep Tayyip Erdoğan wa Uturuki amemwandikia barua Rais Putin akieleza matarajio ya kutatuliwa hali iliyojitokeza katika uhusiano wa nchi hizo mbili baada ya kutunguliwa ndege ya kivita ya Russia.

Katika barua hiyo Recep Tayyip Erdoğan ametuma tena salamu za rambirambi kwa familia ya rubani wa ndege hiyo na kueleza kusitishwa na tukio hilo.

Msemaji wa Ofisi ya Rais wa Uturuki pia amesema, katika barua yake kwa Rais Vladimir Putin, Recep Tayyip Erdoğan ameeleza kukitishwa na tukio la kuangushwa ndege ya Russia na kuiomba radhi familia yake.

Uhusiano wa Moscow na Ankara uliharibika Novemba 2015 baada ya Uturuki kutungua ndege ya kijeshi ya Russia aina ya Sukhoi -24 katika anga ya Syria. Uturuki ilidai kuwa ndege hiyo ya kijeshi iliingia katika anga yake.

Kwa upande wake Moscow ilikadhibisha madai hayo na kuitaka Ankara iombe radhi.

 

Tags