Kushtadi mashambulizi ya kigaidi huko Pakistan; sababu na taathira zake
(last modified Sat, 04 Nov 2023 11:42:09 GMT )
Nov 04, 2023 11:42 UTC
  • Kushtadi mashambulizi ya kigaidi huko Pakistan; sababu na taathira zake

Kitengo cha Mahusiano ya Umma cha Jeshi la Pakistan kimetangaza kuwa vikosi vya jeshi hilo vimesambaratisha shambulio la kigaidi la leo asubuhi katika kambi ya kikosi cha jeshi la anga katika mji wa Mianwali katika jimbo la Punjab. Wavamizi watatu wameuwa na magaidi kadhaa wamekimbia eneo la tukio.

Vyombo vya habari vya Pakistan vimetangaza kuwa magaidi wameharibu ghala dogo la kuhifadhia mafuta na kushambulia ndege tatu mbovu katika tukio la kurushiana risasi. Hata kama mashambulizi ya kigaidi hujiri mara kwa mara huko Pakistan lakini inaonekana kuwa milipuko iliyotokea siku mbili zilizopita na shambulio katika kambi ya kikosi cha anga cha jeshi la Pakistan havipasi kuhusishwa na vitisho vya karibuni vya serikali na jeshi la nchi hiyo kuhusu kuwafukuza wahamiaji haramu nchini humo.  

Hata hivyo, kundi la kigaidi la Tehreek-e-Taliban Pakistan, ambalo limezidisha mashambulizi yake nchini humo katika miezi ya hivi karibuni, inawezekana likatumia nafasi iliyopo kutekeleza mashambulizi ya kigaidi nchini Pakistan ili kuharibu zaidi uhusiano kati ya kundi la Taliban la Afghanistan na serikali ya Islamabad.

Tehreek-e-Taliban Pakistan

Ahmad Mansourkhan mchambuzi wa masuala ya kisiasa anazungumzia hili akisema: "Katika siku za karibuni viongozi mbalimbali wa Taliban ya Afghanistan waliitishia kwa njia mbalimbali serikali ya Pakistan kuhusu kuwafukuza wahamiaji haramu wa Kiafghani. Kwa msini huo, katika mazingira hayo kila kundi linalopinga na adui wa Pakistan linaweza kuzidisha mashambulizi yake na milipuko ya kigaidi dhidi ya jeshi la Pakistan; na hivyo kushadidisha hali ya mgogoro katika uhusiano wa pande mbili ingawa kundi la kigaidi la Tehreek-e-Taliban bado limeazimia kushadidisha hujuma zake.  

Hata kama hadi sasa hakuna mtu au kundi lolote lililotangaza rasmi kuhusika na hujuma ya kigaidi katika kambi ya kikosi cha anga cha jeshi la Pakistan lakini inaelezwa kuwa kundi moja la kigaidi lenye mfungamano na Tehreek-e-Taliban ya Pakistan kwa jina la Tehreek-e- Jihad la Pakistan limekiri kuhusika na shambulio hilo; hatua ambayo inaweza kuwa ni kifuniko tu. Hii ni kwa sababu, kwa kuzingatia uwezo wa kioparesheni na kiitelijinsia wa jeshi la Pakistan; shambulio kama hilo linahitaji nguvu na uwezo wa hali ya juu na haiwezekani vijikundi vidogo na visivyojulikana kuwa na uwezo na zana kama hizo. Pamoja na hayo, magaidi  kivyovyote wanajaribu kulionesha jeshi la Pakistan kuwa ni jeshi dhaifu, linaloweza kupenyeka kwa urahisi na kudhurika. Hii ni kwa sababu, hujuma ya kigaidi ya jana Ijumaa dhidi ya msafara wa askari usalama wa nchi hiyo katika jimbo la Baluchistan huko Pakistan iliyosababisha vifo vya wanajeshi 14 wa nchi hiyo ni jambo lisilokubalika mbele ya fikra za waliowengi nchini humo; kwani jeshi hilo ambalo limejitayarisha kukabiliana na mpinzani wake wa jadi  India, limepata hasara kubwa katika shambulio hilo la kigaidi.

Askari usalama wa Pakistan 

Murtadha Haidar mchambuzi wa masuala ya kisiasa anasema: "Mashambulizi ya kigaidi huko Pakistan ambayo yanatekelezwa kwa sababu na madhumuni tofauti, hayawezi kuhalalisha maafa makubwa ya kuuliwa askari usalama na vikosi vya  jeshi la nchi hiyo.  Hali hii ya mambo inawapa kiburi magaidi cha kuendeleza jinai zao. Hii ni kwa sababu, ni karibu miongo minane sasa ambapo jeshi la Pakistan lina uwezo mkubwa na limejiandaa kieneo kukabiliana na jeshi la India; na kuendelea harakati za makundi ya kigaidi huko Pakistan hakuwezi kuhalalishwa kwa njia yoyote ile. 

Ala Kulli haal, kuwepo anga na mazingira mazuri kwa magaidi kuathiri maamuzi yoyote ya serikali ya Pakistan kutawafanya wazidi kuwa na kiburi na hivyo kuendeleza hujuma zao nchini humo. Hata kama ni vigumu kudhibiti maeneo ya kikabila ya Pakistan kwa upande wa kijiografia, mazingira ya kikabila na kikaumu lakini kudhurika na kupata pigo jeshi na vikosi vya usalama vya Pakistan mkabala wa vitisho vyovyote au mashambulizi ya kigaidi kunaweza kuathiri utendaji wa serikali ya Islamabad kuhusu maamuzi yoyote ya kikanda na kimataifa; ambayo si kwa maslahi ya Pakistan katika makabiliano yake na hasimu wake wa kikanda na kinyuklia. Kwa msingi huo, ushirikiano wa kikanda wa jeshi la Pakistan kwa ajili ya kuwaangamiza magaidi na kurejesha amani na usalama wa kudumu nchini humo bila shaka unaweza kuwakatisha tamaa magaidi na kuandaa pia uwanja wa kutelekezwa mipango ya ustawi na maendeleo nchini humo.