Iceland yapiga kura ya kususia bidhaa za Israel
https://parstoday.ir/sw/news/world-i10546-iceland_yapiga_kura_ya_kususia_bidhaa_za_israel
Mji mkuu wa Iceland umetangaza kuwa wakazi wake wamepiga kura ya kuunga mkono kususiwa bidhaa zinazozalishwa na utawala wa Kizayuni wa Israel hadi pale Palestina itakapotangazwa kuwa taifa huru.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 04, 2016 02:46 UTC
  • Iceland yapiga kura ya kususia bidhaa za Israel

Mji mkuu wa Iceland umetangaza kuwa wakazi wake wamepiga kura ya kuunga mkono kususiwa bidhaa zinazozalishwa na utawala wa Kizayuni wa Israel hadi pale Palestina itakapotangazwa kuwa taifa huru.

Wakazi wa Manispaa ya Mji Mkuu wa Iceland, Reykjavik jana Jumapili walipiga kura ya kuunga mkono kususiwa bidhaa za Israel katika mji huo. Kura hiyo ni katika mikakati ya harakati ya mashirika 170 ya Palestina inayojulikana kama Boycott, Divestment and Sanctions (BDS), iliyoanza kushinikiza kususiwa bidhaa za Tel Aviv mwaka 2005, hadi pale itakapotekeleza wajibu wake kwa msingi wa sheria za kimataifa. Mapema mwezi Aprili mwaka huu, Umoja wa Ulaya ulitakiwa kususia bidhaa zinazozalishwa na utawala wa Kizayuni wa Israel. Wito huo ulitolewa na Rami Hamdallah, Waziri Mkuu wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina alipokutana na kufanya mazungumzo na Chistian Berger, Mkurugenzi wa Masuala ya Mashariki ya Kati katika Taasisi ya Masuala ya Nje ya Ulaya EEAS, huko mjini Ramallah katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan. Hamdallah alizitaka nchi zote za Ulaya kusimamisha uagizaji wa bidhaa zinazozalishwa na utawala haramu wa Israel ndani ya ardhi za Palestina unazozikalia kwa mabavu.