Dec 09, 2023 02:27 UTC
  • Putin kugombea kiti cha urais mwakani

Rais Vladimir Putin wa Russia ambaye duru yake ya kisheria ya urais inamalizika mwanzoni mwa mwezi Mei mwaka kesho, ametangaza kuwa atagombea tena kiti cha urais mwaka kesho, 2024.

Artem Zhoga, Spika wa Jamhuri ya Donetsk amemwomba Putin agombee tena kiti cha urais katika uchaguzi ujao wa Russia. Putin pia amemjibu Zhoga na kutangaza kuwa amekubali ombi hilo na kwamba atagombea tena kiti cha urais Russia. 

Muhula wa uongozi wa Rais Putin unamalizika Mei 7 mwaka kesho na uchaguzi wa rais wa Russia umepangwa kufanyika Machi 17 mwaka kesho.  Dmitry Peskov, msemaji wa Ofisi ya Rais wa Russia (Kremlin) amesema kuhusu suala hili kwamba: Matamshi ya Putin kuhusu uamuzi aliochukua wa kugombea tena kiti cha urais mwakani ni jibu kwa matakwa mengi katika uwanja huo. 

Dmitry Peskov

Peskov amekumbusha kuwa Putin bado hajaanza rasmi kampeni za uchaguzi kwa sababu bado hajajiandikisha kuwa mgombea katika uchaguzi ujao wa rais.