Wamarekani wengi hawataki Joe Biden agombee tena urais
(last modified Tue, 13 Feb 2024 02:25:57 GMT )
Feb 13, 2024 02:25 UTC
  • Wamarekani wengi hawataki Joe Biden agombee tena urais

Matokeo ya uchunguzi mpya wa maoni uliofanyika nchini Marekani yanaonesha kuwa wananchi wengi wa nchi hiyo wanapinga Joe Biden, rais wa nchi hiyo kushiriki katika uchaguzi ujao wa rais ambao unatarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu wa 2024.

Shirika la habari la FARS limeripoti habari hiyo na kunukuu matokeo ya uchunguzi mpya uliofanywa na ABC na Taasisi ya Utafiti ya Ipsos ambayo yanaonesha kuwa, asilimia 86 ya Wamarekani wanaamini kuwa rais wa hivi sasa wa Marekani, Joe Biden, ni kizee mno na hana hadhi ya kuendelea kuweko kwenye Ikulu ya nchi hiyo. 

Hivi karibuni, Robert Hoare, mchunguzi maalumu wa Idara ya Mahakama ya Marekani alitangaza kuwa, "Biden hata hakumbuki ni lini mtoto wake alikufa au zama alipokuwa makamu wa rais wa Obama."

Joe Biden, rais kizee wa Marekani asiye na kumbukumbu 

 

Katika kipindi cha miezi ya hivi karibuni, mchunguzi maalumu wa Idara ya Mahakama ya Marekani amekuwa akifuatili kesi ya kupatikana nyaraka za siri katika nyumba na ofisi binafsi ya Biden.

Katika ripoti yake ya hivi karibuni, Robert Hoare, alimtaja Joe Biden kuwa mtu kizee, anayevaa vizuri mwenye kumbukumbu dhaifu. Alisema, kuna uwezekano Biden hata amesahau ni lini alisahau nyaraka za siri kwenye maegesho ya magari ya nyumbani kwake. 

Wakati wasiwasi huo mkubwa ukiongezeka nchini Marekani kuhusu afya ya Joe Biden, "Ronnie Jackson," mjumbe wa chama cha Republican wa Baraza la Wawakilishi la Marekani ambaye pia ni daktari wa zamani wa White House, ametoa mwito wa kuuzuliwa mara moja Biden kutokana na ulemavu wa kimwili na kiakili wa rais huyo wa Marekani.

Tags