Mar 15, 2024 07:40 UTC
  • Zoezi la upigaji kura kumchagua rais wa Russia limeanza leo

Zoezi la upigaji kura wa nchi nzima wa kumchagua rais wa Russia limeanza rasmi leo.

Kwa mujibu wa IRNA, milango ya vituo 200 vya kupigia kura huko Kamchatka na vituo 55 vya kupigia kura huko Chukotka mashariki mwa Russia vilifunguliwa kwa wapiga kura asubuhi ya leo Ijumaa ili kupokea wapiga kura kwa muda wa siku tatu kama ilivyo katika mikoa mingine ya nchi hiyo.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, jumla ya vituo 93,920 vimepangwa kwa ajili ya kupiga kura kwa raia wa Russia, ambapo vituo 93,644 viko ndani na vituo 269 viko nje ya nchi hiyo, na vituo saba vya kupigia kura viko kwenye kituo cha anga cha Baikonur.

Vladimir Putin (rais wa sasa), Nikolai Kharitonov (wa Chama cha Kikomunisti), Vladislav Davankov (wa Chama Kipya cha Wananchi) na Leonid Slutsky (wa Chama cha Demokrasia ya Kiliberali) ndio wanaowania urais katika uchaguzi huo.

Kulingana na shirika la habari la TASS, watu milioni 114, 212, 734 wametimiza masharti ya kupiga kura katika uchaguzi wa rais ambapo milioni 112, 309, 947 wanaishi nchini Russia.

Idadi ya raia wa Russia walioko nje ya nchi waliotimiza masharti ya kupiga kura katika uchaguzi huu ni 1,890,863.../

 

Tags