Apr 29, 2024 07:01 UTC
  • Wanafunzi wanaunga mkono Palestina waendelea kukamatwa Marekani

Katika siku za hivi karibuni, polisi nchini Marekani wamewatia mbaroni wanafunzi wa vyuo vikuu wasiopungua 900 wanaoiunga mkono Palestina na wanaopinga mauaji ya kimbari ya utawala ghasibu na haramu wa Israel katika Ukanda wa Gaza

 Vyuo vikuu vya  Marekani vimeshuhudia maandamano ya nchi nzima ya wanachuo wa vyuo vikuu na maprofesa wakilalamikia siasa za Washington za kuunga mkono utawala haramu wa Kizayuni katika vita dhidi ya Ukanda wa Gaza.

Pamoja na kuongezeka kwa wingi na ukubwa wa maandamano, wasimamizi wa vyuo vikuu vya Marekani wamekandamiza waandamanaji wa wanafunzi wa vyuo vikuu kwa njia ambazo hazijawahi kushuhudiwa katika nchi hiyo.

Wanafunzi hao wa vyuo vikuu vya Marekani na maprofesa  wengi na washiriki wote wamekamatwa kwa wingi  katika maandamano hayo.

Kwa mujibu wa gazeti la Washington Post, kufuatia vuguvugu la kushikamana na watu wa ukanda wa Gaza na maandamano katika vyuo vikuu vya Marekani, yaliyoanzia Chuo Kikuu cha Columbia huko New York na kuenea katika vyuo vikuu vingine vya nchi hiyo na duniani kote, takribani watu mia tisa 900 wameshakamatwa na Vyuo vikuu 15 vya nchi hiyo katika kipindi cha siku 10 zilizopita.

 

Katika kuiunga mkono Palestina na kupinga jinai zinazofanywa na utawala haramu wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza, wanafunzi hao walidai kutoshirikiana na makampuni yanayopata faida kutoka kwa utawala huo ghasibu.

Utawala huo haramu wa  Kizayuni  kwa uungwaji mkono na Marekani na mbele ya macho ya haki za binadamu na mashirika ya kimataifa umekuwa ukifanya mauaji ya kimbari dhidi ya watu wasio na ulinzi wa eneo hilo na  kwa kushambulia ukanda wa Gaza kwa zaidi ya miezi sita.

Katika kipindi hiki wanachofanya mashambulizi, utawala bandia wa Israel haujapata mafanikio yoyote isipokuwa jinai, mauaji, uharibifu, jinai za kivita, ukiukaji wa sheria za kimataifa, ulipuaji wa mashirika ya misaada.