May 01, 2024 06:50 UTC

Wananchi wa miji tofauti ya dunia kwa mara nyingine wameandamana kuwatetea wananchi madhulumu wa Palestina na kulaani jinai za utawala ghasibu wa Israel katika Ukanda wa Gaza.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Iran (IRNA), wanafunzi wa vyuo vikuu vya  Ugiriki wanaoiunga mkono Palestina na Ukanda wa Gaza wamefanya maandamano mbele ya ubalozi wa utawala ghasibu wa Israel huko Athens na kutaka kusitishwa mashambulizi ya utawala huo wa Kizayuni unaofanya mauaji ya kimbari huko Gaza haraka iwezekanavyo

Wanafunzi wa vyuo vikuu vya Lebanon pia wamemenya maandamano ya kuwaunga mkono wananchi wa Palestina hasa wakazi wa Ukanda wa Gaza na kulaani mauaji ya kimbari yanayofanywa na utawala ghasibu wa Israel.

Marekani" na "mauti kwa Israel".Wanafunzi hao waliokuwa wamebeba bendera za Lebanon na Palestina, wametoa nara za "mauti kwa Marekakni" na mauti kwa Israel".

Maandamano ya kuwatetea Wapalestina barani Ulaya

chini Ufaransa pia wanafunzi wa vyuo vikuu wamefanya maandamano kwa siku kadhaa mfululizo kuwaunga mkono watu wa Ukanda wa Gaza. Jumatatu wiki hii wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sorbonne mjini Paris, walifanya maandamano na kutundika bendera za Palestina kwenye majengo ya chuo hicho.

Maandamano kama hayo ya wanafunzi wa vyuo vikuu kuwaunga mkono na kuwatetea watu wa Gaza wanaoendelea kuuawa na jeshi la Israel yameshuhudiwa pia katika nchi za Mauritania, Iran, Pakistan Mexico.

Jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina zimechochea hasira na hisia kali za walimwengu, na katika maeneo yote ya duniani, serikali na taasisi mbalimbali za kimataifa zimetoa wito wa kuwaunga mkono wananchi madhulumu wa Palestina huko ukanda wa Gaza.

Tags