Jesi la Uturuki lasema limechukua madaraka ya nchi ili kulinda demokrasia
https://parstoday.ir/sw/news/world-i11323-jesi_la_uturuki_lasema_limechukua_madaraka_ya_nchi_ili_kulinda_demokrasia
Jeshi la Uturuki limesema kuwa, limechukua madaraka ya nchi hiyo na kuiondoa madarakani serikali ya Rais Recep Tayyip Erdogan na kwamba litalinda utawala wa sheria nchini humo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 15, 2016 17:21 UTC
  • Jesi la Uturuki lasema limechukua madaraka ya nchi ili kulinda demokrasia

Jeshi la Uturuki limesema kuwa, limechukua madaraka ya nchi hiyo na kuiondoa madarakani serikali ya Rais Recep Tayyip Erdogan na kwamba litalinda utawala wa sheria nchini humo.

Televisheni ya taifa ya Uturuki imetangaza habari hiyo na kuongeza kuwa, mkuu wa jeshi la nchi hiyo Hulusi Akar anashikiliwa na wanajeshi waliofanya mapinduzi.

Televisheni ya al Alam imemnukuu Rais Erdogan akisema kwa njia ya simu kuwa waliofanya mapinduzi hayo watashindwa, na kutoa mwito wa watu kumiminika mitaani.

Shirika la habari la AFP limetangaza kutokea miripuko miwili mikubwa katika kituo cha mafunzo ya polisi.

Milio ya risasi imesikika muda mchache katika maeneo tofauti ya Uturuki.

Hadi tunaandaa habari hii, hali nchini ilikuwa ni tata na habari za kugongana zinaendelea kuripotiwa kutoka nchini humo.