Jul 29, 2024 02:56 UTC
  • Ulaya yaendelea kushuhudia maandamano ya kuwaunga mkono Wapalestina

Wananchi wa nchi mbalimbali za barani Ulaya kwa mara nyingine wamefanya maandamano ya kuwaunga mkono wananchi madhulumu wa Gaza, Palestina.

Kundi kubwa la wananchi wa Ujerumani wamefanya maandamano mjini Berlin, mji mkuu wa nchi hiyo na kutaka kuharakishwa hatua za kisheria za kumkamata Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala bandia wa Israel kwa tuhuma za kufanya mauaji ya halaiki katika Ukanda wa Gaza.

Wafuasi wa Palestina nchini Sweden pia wamelaani kuendelea mauaji ya halaiki katika Ukanda wa Gaza yanayofanywa na utawala wa Israel unaoua watoto kwa kukusanyika mbele ya ubalozi wa Marekani mjini Stockholm.

Wananchi wa Uturuki pia wamefanya maandamano katika miji tofauti ya nchi hiyo kwa ajiilii ya kuwaunga mkono wananchi madhulumu wa Palestina na kulaani jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Gaza.

 

Maandamano kama hayo yameshuhuhudiwa pia katika mataifa mengine barani Ulaya na kuzidi kuonyesha kwamba, walimwengu wameamka, kwani hata katika mataifa ambayo serikali zake zinaunga mkono Israel na hata kuupatia silaha utawala huo kama Ujerumani, Marekani na Uingereza kumekuwa kukishuhudiwa wimbi kubwa la maandamano ya kulaani jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel.

Hayo yanajiri katiika hali ambayo, eneo la Ukanda wa Gaza linakabiliwa na "hali mbaya zaidi ya ukosefu wa chakula" na kwamba hadi kufikia mwisho wa 2023, wakazi wote milioni 2.2 wa eneo hilo walihesabika kuwa ni watu walio katika hatua ya tatu au zaidi ya hali "mbaya sana" kwa mtazamo wa usalama wa chakula.

Tags