Athari za jinai za Marekani nchini Afghanistan
https://parstoday.ir/sw/news/world-i115306-athari_za_jinai_za_marekani_nchini_afghanistan
Kundi la Taliban linaloongoza Afghanistan limetoa taarifa likitaja maadhimisho ya kumbukumbu ya kuondoka Marekani nchini humo kuwa ni muhimu, fakhari na Siku ya ushindi kwa nchi hiyo.
(last modified 2024-08-17T00:52:32+00:00 )
Aug 17, 2024 00:52 UTC
  • Athari za jinai za Marekani nchini Afghanistan

Kundi la Taliban linaloongoza Afghanistan limetoa taarifa likitaja maadhimisho ya kumbukumbu ya kuondoka Marekani nchini humo kuwa ni muhimu, fakhari na Siku ya ushindi kwa nchi hiyo.

Marekani iliivamia na kuikalia kwa mabavu Afghanistan mwaka 2001 kwa kisingizio kuwa nchi hiyo imewapa hifadhi wanamgambo wa kundi la Taliban lililokuwa likiongozwa na vinara wa al Qaida hasa Osama bin Laden ambaye alituhumiwa kuhusika katika mashambulizi ya anga katika jengo la minara pacha huko Marekani. 

Osama bin Laden 

Kubakia vikosi vamizi vya Marekani pamoja na wanajeshi wa Muungano wa Kijeshi wa Nchi za Magharibi (NATO) huko Afghanistan kwa kwa kipindi cha miongo miwili kulikwenda sambamba na jinai chungu nzima na kuuliwa raia wa nchi hiyo kwa visingizio mbalimbali. Ingawa vyombo vya kujitegemea havijafanya uchunguzi wa kina kuhusiana na suala hili, lakini ripoti chache zilizochapishwa na duru za kujitegemea na baadhi ya duru za Magharibi zimeweka wazi ukatili na uhalifu usiohesabika, hasa uliofanywa na wanajeshi wa Marekani, Uingereza, Australia na Ujerumani huko Afghanistan. 

Amin Farjad mchambuzi wa masuala ya kisiasa anazungumzia suala hili akisema: "Jinai zilizofanywa na vikosi vamizi vya majeshi ya Marekani na Uingereza na muungano wao vamizi huko Afghanistan hazihesabiki. Miongoni mwa jinao hizo tunaweza kuashiria mauaji ya kihholela yaliyokuwa yakifanywa na askari vamizi dhidi ya raia wa Afghanistan ili kujifurahisha na kwa ajili ya burudan tu na kukata vidole vyao kwa ajili ya kuweka takwimu. Aidha tunaweza kuashiria hatua ya wanajeshi vamizi wa Marekani na washirika wake ya kukata vipande vipande miili ya raia waliowauwa na kisha kuanzisha jela binafsi ili kufurahia mateso ya wananchi wa Afghanistan." 

Sambamba na jinai hizo, kitendo cha wanajeshi vamizi cha kuingia nyakati za usiku katika nyumba za wananchi wa Afghanistan, jambo ambalo ni kinyume kabisa na utamaduni na mila yao ya kitaifa ya Kiislamu, pamoja na kuwatia nguvuni na kuwanyonga watu kiholela ilikuwa sehemu nyingine ya jinai za vikosi vamizi katika miongo miwili ya kuikalia kwa mabavu Afghanistan. Matumizi ya mabomu yaliyopigwa marufuku kama yale ya mada ya fosforasi nyeupe yalisabisha magonjwa mbalimbali yasiyoweza kutibika huko Afghanistan na hadi sasa watu wa nchi hiyo wanaendelea kutaabika na kusumbuliwa na athari za maradhi hayo. Mbali na hili, hatua ya vikosi vamizi ya kutumia aina mbalimbali za mabomu yenye nguvu kubwa yakiwemo yale yaliyopewa jina la Mama wa Mabomu Yote (GBU-43/B MOAB) huko Toura Bora imeacha athari mbaya sana kwa mazingira, hasa katika ardhi ya kilimo. Wakati huo huo, mabomu ya kutegwa chini ya ardhi yaliyobaki wakati wa kukaliwa kwa mabavu Afghanistan yanaendelea kuwa tishio kwa maisha ya Waafghani hasa watoto. Maelfu ya watu nchini humo wameuliwa au kuwa vilema kutokana na mabomu hayo ya kutegwa ardhini. 

Zama za vikosi vamizi vya Marekani nchini Afghanistan 

Ala kulli hal, mbali na mauaji, mienendo ya utovu wa maadili ya umma na uchomaji moto wa nakala za Qurani Tukufu vilivyofanywa na wanajeshi vamizi wa nchi za Maghahribi huko Afghanistan, suala la dawa za kulevya ni tatizo jingine lililosabishwa na uvamizi wa Marekani na  NATO huko Afghanista, iwe ni katika uzalishaji au katika kuendesha biashara hiyo haramu. Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA) lilitumia madawa ya kulevya kama sehemu ya vyanzo vya fedha vya nchi hiyo huko Afghanistan. jambo hili lilipelekea kuongezeka pakubwa uzalishaji wa mihadarati nchini Afghanistan kwa njia za kienyeji na viwandani.

Maafa na taathira nyingine zilizoachwa kufuatia uvamizi wa Marekani na NATO huko Afghanistan ni kuwafanya watu wa nchi hiyo kuwa waraibu wa mihhadarati hususan tabaka la vijana ambao walikuwa wakitumia dawa aina ya heroine na aina nyingine za mihadarati ya viwandani iliyoathiri karibu wanawake na wanaume milioni tatu nchini humo na kuwa tatizo kubwa kwa jamii.

Kwa hiyo, taathira za jinai za vikosi vya majeshi vamizi vya Marekani na NATO na maafa na uharibifu mkubwa na uvamizi huo vinahitajia uchunguzi huru na kuwasilishwa suala hili katika mahakama stahiki ya kimataifa. Ingawa kumefunguliwa kesi kadhaa katika uwanja huu aghalabu zikiwa kwa ajili ya kuwaghafilisha wananchi wa Afghanistan na kupunguza malalamiko ya watu katika ngazi ya kikanda, lakini kesi hizo si tu kuwa hazijafuatiliwa kwa umakini bali wahusika wa jinai hizi pia wameondolewa hatiani.