Uholanzi yalaani ukatili wa Wazayuni dhidi ya Wapalestina
https://parstoday.ir/sw/news/world-i115320-uholanzi_yalaani_ukatili_wa_wazayuni_dhidi_ya_wapalestina
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Uholanzi amelaani mashambulizi ya walowezi wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na kutaka ulinzi wa raia.
(last modified 2024-08-17T03:51:27+00:00 )
Aug 17, 2024 03:39 UTC
  • Uholanzi yalaani ukatili wa Wazayuni dhidi ya Wapalestina

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Uholanzi amelaani mashambulizi ya walowezi wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na kutaka ulinzi wa raia.

Caspar Veldkamp, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Uholanzi amesema: Ninalaani ghasia zilizofanywa na walowezi wenye itikadi kali dhidi ya Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi. Mamlaka za Israel lazima zichukue hatua kulinda jamii na kuzuia vurugu.

Siku ya Alhamisi usiku, zaidi ya walowezi mia moja wa Israel walishambulia kijiji cha Jit karibu na mji wa Qalqilya na kuchoma moto nyumba na magari ya Wapalestina. Kwa mujibu wa tangazo la Wizara ya Afya ya Palestina, Mpalestina mmoja aliuawa kwa kupigwa risasi na walowezi wa Israel waliokuwa wamavaa barakoa, na mtu mwingine kujeruhiwa.

Sammba na jinai za Israel walowezi wa Kizayuni wameendelea kuvamia msikiti wa al-Aqswa na kufanya vitendo vya kichochezi.

Caspar Veldkamp, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Uholanzi

 

Hivi kkaribuni, walowezi wa utawala haramu wa Israel wamevamia boma la Msikiti wa al-Aqsa, huku waziri mkaidi mwenye siasa kali za mrengo wa kulia wa utawala huo Itamar Ben-Gvir akijiunga nao na hivyo kuzua mvutano mpya na Waislamu Wapalestina ambao hutekeleza ibada katika eneo hilo takatifu.

Zaidi ya walowezi 1,600 wa Israel, ambao walipangwa katika makundi 13, walivamia Msikiti wa al-Aqsa katika mji mtakatifu wa Quds (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu na Israel Jumanne asubuhi.