Maandamano ya kuiunga mkono Palestina yafanyika Chicago
https://parstoday.ir/sw/news/world-i115424-maandamano_ya_kuiunga_mkono_palestina_yafanyika_chicago
Katika kukaribia kufanyika kongamano la kitaifa la chama cha Democrat nchini Marekani idadi kubwa ya wananchi wanaopinga sera za kupenda vita za serikali ya Washington na uungaji mkono wake kwa utawala wa Kizayuni katika vita vya Gaza wameandamana katika mji wa Chicago kwa lengo la kuiunga mkono Palestina na kulaani jinai za utawala ghasibu wa Kizayuni.
(last modified 2024-08-19T23:14:17+00:00 )
Aug 19, 2024 23:14 UTC
  • Maandamano ya kuiunga mkono Palestina yafanyika Chicago

Katika kukaribia kufanyika kongamano la kitaifa la chama cha Democrat nchini Marekani idadi kubwa ya wananchi wanaopinga sera za kupenda vita za serikali ya Washington na uungaji mkono wake kwa utawala wa Kizayuni katika vita vya Gaza wameandamana katika mji wa Chicago kwa lengo la kuiunga mkono Palestina na kulaani jinai za utawala ghasibu wa Kizayuni.

Mamia kadhaa ya raia wa Marekani hususan shakhsia wa Kiislamu na washirika wao wanaochukizwa na uungaji mkono wa serikali ya Marekani kwa mashambulizi ya utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza na kuongezeka idadi ya vifo vya raia, wanataka kutazamwa upya sera za chama cha Democrat.  

Waandamanaji wamepanga kukishinikiza chama hicho ili kuwekewa vikwazo vya silaha Tel Aviv. 

Waandamanaji wanazidisha mashinikizo kwa chama cha Democrat katika hali ambayo chama hicho kimeanza kongamano lake la kitaifa tangu jana huko Chicago. Kongamano hilo litaendelea hadi   tarehe 22 mwezi huu wa Agosti.