Jaribio la mapinduzi Uturuki; 50,000 wakamatwa na kupigwa kalamu
https://parstoday.ir/sw/news/world-i11605-jaribio_la_mapinduzi_uturuki_50_000_wakamatwa_na_kupigwa_kalamu
Jaribio la mapunduzi ya kijeshi lililofeli nchini Uturuki limesababisha wafanyakazi 45,000 wa serikali kupigwa kalamu nyekundu huku wengine zaidi ya 5,000 wakizuiliwa kwa tuhuma za kuhusika na mapinduzi hayo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 20, 2016 03:07 UTC
  • Jaribio la mapinduzi Uturuki; 50,000 wakamatwa na kupigwa kalamu

Jaribio la mapunduzi ya kijeshi lililofeli nchini Uturuki limesababisha wafanyakazi 45,000 wa serikali kupigwa kalamu nyekundu huku wengine zaidi ya 5,000 wakizuiliwa kwa tuhuma za kuhusika na mapinduzi hayo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, serikali ya Rais Reccep Teyyip Erdogan imewasweka korokoroni na kuwafuta kazi watumishi wa umma wanaoaminika kuhusika kwa njia moja au nyingine katika mapinduzi hayo, wakiwemo wanajeshi, majaji, walimu, wahadhiri na waandishi wa habari15,000. Tayari vituo kadhaa vya radio na televisheni vya nchi hiyo vimefungwa. Miongoni mwa vyombo vya habari vilivyofungwa ni pamoja na STV, Samanyolu Haber, Samanyolu Haber Radyo, Kanal Türk, Kanal 124, Yumurcak TV, Burç FM, Radyo Mehtap. Licha ya makelele ya jamii ya kimataifa na watetezi wa haki za binadamu, Rais Erdogan amesisitiza kuwa, serikali ya Ankara inatathmini kwa uzito suala la kurejesha adhabu ya kifo.Hii ni katika hali ambayo, Rais Bashar al-Assad wa Syria hivi karibuni alionya kuwa, huenda Rais Reccep Teyyip Erdogan wa Uturuki akatumia jaribio la mapinduzi yaliyofeli kuwaadhibu na kuwaondoa serikalini wakosoaji na wapinzani wake. Rais wa Syria amesema jaribio la mapinduzi ya kijeshi na matukio ya hivi sasa nchini Uturuki yamezungukwa na utata na siri kubwa na kusisitiza kuwa, huenda Rais Erdogan akayatumia matukio hayo kuwaondoa wapinzani wake kwenye taasisi za serikali kama mahakama na jeshi la nchi hiyo.Watu zaidi ya 300 waliuawa katika jaribio hilo la mapinduzi ya kijeshi lililogonga mwamba.