Tabribani watu 300 wafariki Myanmar kwa Kimbunga Yagi
https://parstoday.ir/sw/news/world-i116592-tabribani_watu_300_wafariki_myanmar_kwa_kimbunga_yagi
Idadi ya waliofariki dunia kutokana na Kimbunga Yagi nchini Myanmar imefikia watu 293, huku wengine 89 wakiwa hawajulikani walipo.
(last modified 2024-09-21T01:00:53+00:00 )
Sep 21, 2024 01:00 UTC
  • Tabribani watu 300 wafariki Myanmar kwa Kimbunga Yagi

Idadi ya waliofariki dunia kutokana na Kimbunga Yagi nchini Myanmar imefikia watu 293, huku wengine 89 wakiwa hawajulikani walipo.

Hayo yameelezwa na utawala wa kijeshi wa nchi hiyo ya kusini mwa Asia, huku vyombo vya habari vikiripoti kuwa msaada wa kwanza wa kigeni umeanza kuwasili nchini humo.

Zaidi ya ekari 660,000 za mpunga na mazao mengine ziliharibiwa na mafuriko huku wanyama zaidi ya 100,000 wakifariki.

Kimbunga Yagi kiliyapiga maeneo ya kaskazini mwa mataifa ya Vietnam, Laos, Thailand na Myanmar zaidi ya wiki moja iliyopita.

Mafuriko makubwa na maporomoko ya ardhi kutokana na mvua hiyo yamesababisha vifo vya watu 613 katika eneo hilo.

Wakati huo huo, chombo cha habari kinachoendeshwa na serikali nchini Vietnam kinasema watu 254 wamethibitishwa kufariki na 82 hawajulikani walipo baada ya kimbunga Yagi kuikumba nchi hiyo wiki moja iliyopita.

 

Mamlaka za Vietnam zinasema kimbunga hicho kimefanya uharibifu mkubwa zaidi katika kipindi cha miaka 60.

Kimbunga chenye nguvu zaidi nchini Vietnam katika kipindi cha miaka 30 kimesababisha maafa kote kaskazini mwa nchi hiyo, na kuwaacha watu milioni 1.5 bila umeme.

Ingawa sasa nguvu yake imedhoofika katika hali ya unyogovu wa kitropiki, lakini mamlaka imeonya Yagi kitaleta usumbufu zaidi kinapoelekea magharibi.