Wanajeshi zaidi ya elfu 4 wa Uingereza watoroka jeshini
(last modified 2024-10-19T03:04:19+00:00 )
Oct 19, 2024 03:04 UTC
  • Wanajeshi zaidi ya elfu 4 wa Uingereza watoroka jeshini

Bunge la Uingereza limetangaza kuwa zaidi ya wanajeshi 4,400 wamejiuzulu katika jeshi la nchi hiyo.

Bunge la Uingereza limetangaza kuwa, kufuatia sera za serikali ya nchi hio tangu 2010, jeshi halina uwezo wa kupambana katika vita vya ana kwa na jeshi la nchi nyingine kwa zaidi ya miezi miwili tu kutokana na sera za serikali tangu mwaka 2010.   

Kwa kutegemea takwimu za Wizara ya Ulinzi ya nchi hiyo, Bunge la Uingereza limetangaza kuwa mwaka jana idadi ya watu waliojiunga na jeshi la Uingereza ilikuwa  ndogo kulinganisha na idadi ya askari walioondoka jeshini.

Vyombo vya habari vya Uingereza vimeripoti kuwa, idadi ya askari jeshi wanaokimbia jeshi imegezeka kutokana na kuongezeka mashinikizo kwa askari jeshi na wakati huo huo wanajeshi wanaoajiriwa jeshini wamepungua kwa kiasi kikubwa. 

Kutokana na kusita wananchi nchini Uingereza kujiunga na jeshi na polisi ya nchi hiyo, viongozi wa serikali ya London wanajaribu njia mbalimbali kuwahimiza vijana kujiunga na jeshi na polisi ikiwa ni pamoja na kuwoangezea mishahara askari jeshi na polisi; Hata hivyo weledi wa mambo wanasema kuwa jeshi la Uingereza hadi sasa limefeli katika uwanja huo. 

Matabaka mbalimbali ya wananchi wa Uingereza, wamekuwa wakipaka rangi nyekundu katika jengo a Wizara ya Ulinzi ya nchi hiyo na kuitaja serikali ya London kuwa ni mshirika katika jinai zinazofanywa na utawala wa Kizayuni wa Isarel huko Palestina na Lebanon. 

Waandamanaji wakiwa wamepaka rangi nyekundu katika jengo la Wizara ya Ulinzi ya Uingereza 

Waingereza pia wameitaka serikali ya London isitishe misaada yake ya silaha, intelijinsia na ya kijeshi kwa utawala wa Kizayuni.  

Tags