Russia yataka kuhuishwa makubaliano ya JCPOA
(last modified Fri, 14 Mar 2025 02:30:17 GMT )
Mar 14, 2025 02:30 UTC
  • Russia yataka kuhuishwa makubaliano ya JCPOA

Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia, Sergei Lavrov amesisitiza uungaji mkono wa Moscow kwa kufufuliwa mkataba wa kihistoria uliotiwa saini na Iran na mataifa mengine sita yenye nguvu duniani mwaka 2015.

Lavrov amesema hayo wakati wa mahojiano na wanablogu wa Kimarekani na iusisitiza kuwa,"Tulijadili hali katika Ghuba ya Uajemi pamoja na Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA)."

Sirika la habari la TASS limeripoti habari hiyo na kueleza kuwa, Lavrov alisema hayo akijibu swali ikiwa suala la Iran ni sehemu ya mazungumzo yanayoendelea kati ya Russia na Marekani.

Mwanadiplomasia huyo mkuu wa Russia ameeleza kuwa, "Moscow itaunga mkono kurejelea muundo ambao lipelekea kufikiwa makubaliano ya awali yaliyoidhinishwa na Baraza la Usalama (la Umoja wa Mataifa) na Iran."

"Tutaona jinsi itakavyokuwa," ameongeza Lavrov, akimaanisha mashauriano yanayoendelea kati yake na maafisa wa Marekani na Ulaya.

Hivi karibuni, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia, Maria Zakharova alisema Moscow itshirikiana na Marekani katika kushughulikia masuala ya Asia Magharibi, ikiwa ni pamoja na mradi wa nyuklia wa Iran, ikizingatiwa kuwa uhusiano wa Moscow na Washington unazidi kuimarika.

Alisema mtazamo wa pamoja kwa makubaliano ya nyuklia ya Iran ya mwaka 2015, unaoitwa rasmi Mpango Kamili wa Utekelezaji wa Pamoja (JCPOA), unaweza kuwa na manufaa kwa ajili ya kuleta utulivu katika eneo.