Macron: Kuitambua rasmi Palestina kama nchi huru ni jambo la dharura
Kufuatia kushadidi mashambulio ya Israel dhidi ya Gaza, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, amesisitiza haja ya kutambuliwa rasi Palestina kama taifa.
Wakati wa ziara yake nchini Singapore leo (Ijumaa), amewataka Wazungu kuchukua msimamo wa pamoja dhidi ya Israel na kuainisha masharti ya kuitambua Palestina.
Msimamo wa Macron unaweza kubadilisha diplomasia ya Ulaya kuhusu Palestina na kuathiri uhusiano wa kikanda. Kauli yake pia inaakisi mabadiliko katika sera za Magharibi kuelekea Israel na kuangazia mzozo wa kibinadamu huko Gaza.
Katika wiki za hivi karibuni, nchi za Magharibi, isipokuwa Marekani zimejitenga na Israel.
Viongozi wengine wa Ulaya hata wameibua wasiwasi juu ya uwezekano wa kutengwa kwa Israel kimataifa. Kwa kutetea kutambuliwa kwa Palestina, Ufaransa inataka kuongeza shinikizo kwa Israel.
Ikumbukwe kuwa, Rais wa Ufaransa alitangaza katikati ya mwezi huu wa Aprili kwamba, nchi yake inaweza kuitambua nchi huru ya Palestina Juni ijayo sabamba na kufanyika mkutano kuhusu Palestina huko New York, kitendo ambacho kilimkasirisha Netanyahu. Hadi sasa nchi ya Palestina imetambuliwa na takriban nchi 150 duniani, ingawa nchi nyingi kubwa za Magharibi, zikiwemo Marekani, Uingereza, Ufaransa, Ujerumani na Japan bado hazijachukua hatua hiyo.
Huku mashambulizi ya mara kwa mara katika Ukanda wa Gaza yakiingia mwezi wake wa ishirini, nchi nne za Ulaya za Uhispania, Ireland, Slovania na Norway zimetoa taarifa ya pamoja ya kutaka uanachama kamili wa Palestina katika Umoja wa Mataifa.