Zelensky ataka afanye mazungumzo binafsi na Putin
Rais Vladimir Zelensky wa Ukraine kwa mara nyingine ametoa wito wa kufanyika mazungumzo binafsi kati yake na Rais Vladimir Putin wa Russia, akisema hiyo ndiyo njia pekee ya kupatikana amani ya kudumu.
Hata hivyo Moscow inalichukulia pendekezo hilo kuwa ni jambo lisilo na maana hadi pale wajumbe wa nchi hizo mbili watakapoafikiana kwenye masuala ya msingi.
Siku ya Jumamosi, Zelensky alisema "kasi ya mazungumzo ni lazima iongezwe," na kutaka ifanyike duru mpya ya mazungumzo wiki ijayo - na kwa mara nyingine akadai kufanya mazungumzo binafsi na Putin.
"Kwa kweli mkutano katika ngazi ya viongozi unahitajika ili kuhakikisha amani ya kudumu inapatikana," alisisitiza Zelensky na kuongezea kwa kuse,a: "Ukraine iko tayari."
Muhula wa urais wa Zelensky uliisha mwaka jana, lakini yeye mwenye ameitaja sheria ya kijeshi, ambayo aliiweka, kama sababu za kusalia madarakani.
Hivi karibuni, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia Maria Zakharova alimshutumu mwigizaji huyo wa Ukraine aliyegeuka kuwa mwanasiasa kwa kushinikiza kufanya mazungumzo ya binafsi na Putin akisema ni ya kutaka kujipatia uhalali wa kisiasa, na akaongeza kuwa Zelensky "anaogopa sana kusahauliwa, na kutokuwa na umuhimu kwa nchi za Magharibi"…/