Umoja wa Mataifa unaunga mkono kuanzishwa kwa taifa la Palestina
Msemaji wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa, kwa mtazamo wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, kiwango cha uungwaji mkono mpana kutoka kwa mataifa ya dunia katika suluhu ya mataifa mawili na kuanzishwa kwa taifa huru la Palestina ni muhimu.
Kuhusu kutambuliwa kwa taifa huru la Palestina na baadhi ya nchi za Ulaya na Magharibi, Farhan Haq amesema kuwa, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anatumai kuwa nchi hizo zitatumia kasi iliyoanzishwa katika Mkutano wa Kimataifa wa Palestina (uliofanyika Umoja wa Mataifa kutafuta suluhu linaloweza kufikiwa kwa mzozo wa Israel na Palestina.
Farhan Haq ameongeza kuwa: "Kilicho muhimu kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ni kiwango kikubwa cha uungwaji mkono kutoka kwa nchi zinazoshiriki katika Kongamano la (Kimataifa la Palestina) kwa ajili ya suluhu la mataifa mawili linaloandaliwa na Saudi Arabia na Ufaransa. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anatumai kuwa nchi hizo zitatumia kasi iliyobuniwa kufufua maisha mapya kwenye suluhisho la serikali mbili ili tuweze kuwa na suluhisho linaloweza kufikiwa la serikali mbili."
Hayo yanajiri katika hali ambayo, Markk Carney Waziri Mkuu wa Canada ametangaza kuwa nchi hiyo imepanga kuitambua rasmi nchi ya Palestina katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwezi Septemba mwaka huu.
Awali, Waziri Mkuu wa Uingereza, Keir Starmer pia alisema Jumanne wiki hii kwamba atalitambua taifa la Palestina mwezi Septemba ikiwa utawala wa Israel hautakubali kusitishwa vita huko Gaza na kutumwa misaada ya kibinadamu katika ukanda huo.
Hivi karibuni pia Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa alisema kuwa Paris itaitambua rasmi nchi ya Palestina na kwamba itatangaza rasmi uamuzi huu katika Mkutano wa Baraza Kuu la UN mwezi Septemba.