Taarifa ya Umoja wa Ulaya na nchi tisa ya kupinga kukaliwa kwa mabavu Gaza
https://parstoday.ir/sw/news/world-i129374
Madola tisa ya Magharibi pamoja na Umoja wa Ulaya yametoa taarifa ya kukataa kukaliwa kwa mabavu Gaza na kuutaja mpango huo wa Israel kuwa ni ukiukaji wa sheria za kimataifa na za kibinadamu.
(last modified 2025-08-10T10:24:47+00:00 )
Aug 10, 2025 10:10 UTC
  • Taarifa ya Umoja wa Ulaya na nchi tisa ya kupinga kukaliwa kwa mabavu Gaza

Madola tisa ya Magharibi pamoja na Umoja wa Ulaya yametoa taarifa ya kukataa kukaliwa kwa mabavu Gaza na kuutaja mpango huo wa Israel kuwa ni ukiukaji wa sheria za kimataifa na za kibinadamu.

Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa Austria, Kanada, Ufaransa, Ujerumani, Italia, New Zealand, Norway, Uingereza, Australia, na Mwakilishi Mkuu wa Umoja wa Ulaya wa katika Masuala ya Kigeni na Kiusalama, wametoa taarifa na kupinga vikali uamuzi wa baraza la mawaziri la usalama la Israel wa mnamo tarehe 8 Agosti wa kuanzisha operesheni nyingine kubwa ya kijeshi huko Gaza na kuukalia kwa mabavu ukanda huo.

Wamesema katika taarifa yao kwamba, operesheni hiyo itazidisha hali mbaya ya kibinadamu, kuhatarisha maisha ya mateka na kuongeza hatari ya kuenea kwa raia kukimbia makazi yao.

Taarifa hiyo pia imebainisha kuwa, mpango wa utawala ghasibu wa Israel wa kuikalia kikamilifu Gaza una hatari ya kukiuka sheria za kimataifa za kibinadamu, huku jaribio lolote la kujumuisha au kuendeleza ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi likiwa linakiuka sheria za kimataifa.

Taarifa ya pamoja ya kundi la nchi hizo imesisitiza kuwa: "Wakati hali mbaya zaidi ya njaa ikitokea Gaza, tunatoa wito kwa Israel, Hamas, na jamii ya kimataifa kufanya kila wawezalo ili kukomesha vita hivyo vya kutisha, kwa njia ya usitishaji vita wa mara moja na wa kudumu unaoruhusu kufikishwa kwa misaada ya kibinadamu iliyoenea, ya haraka na isiyozuiliwa."