UNICEF: Watu wanane kati ya kumi nchini Afghanistan wanakunywa maji machafu
https://parstoday.ir/sw/news/world-i133104-unicef_watu_wanane_kati_ya_kumi_nchini_afghanistan_wanakunywa_maji_machafu
Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) limetangaza kuwa, zaidi ya nusu ya vyanzo vya maji vya Afghanistan vimekauka.
(last modified 2025-11-12T23:07:10+00:00 )
Nov 12, 2025 23:07 UTC
  • UNICEF: Watu wanane kati ya kumi nchini Afghanistan wanakunywa maji machafu

Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) limetangaza kuwa, zaidi ya nusu ya vyanzo vya maji vya Afghanistan vimekauka.

UNICEF imeonya kwamba athari za mabadiliko ya tabianchi kwa Afghanistan zimefikia kiwango cha "dharura ya kimya" na zaidi ya nusu ya rasilimali za maji katika mikoa yenye ukame zimekauka.

Ripoti ya Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) inaeleza kuwa, watu wanane kati ya kumi nchini Afghanistan wanakunywa maji ambayo si salamu kwa matumizii ya binadamu.

UNICEF imetangaza kuwa mabadiliko ya tabianchi yamekuwa na athari hasi na kubwa mno kwa maisha ya watu wa Afghanistan, na nchi hiyo sasa inakabiliwa na tatizo kubwa la uhaba wa maji.

Tajuddin Oywal, mwakilishi wa UNICEF nchini Afghanistan, alisema mwanzoni mwa Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi  huko Brazil kwamba, Afghanistan ni moja ya nchi ambazo zinakabiliwa zaidi na mzozo wa hali ya hewa, ingawa nafasi na mchango wowote katika kuuanzisha.

Wakati huo huo, Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) limetangaza kuwa, familia tisa kati ya 10 nchini Afghanistan zinakabiliwa na njaa au zinalazimika kubeba madeni huku raia wakimbizi waliorejea hivi karibuni wakijikimu kimaisha kwa tabu katika maeneo yenye hali mbaya ya umaskini mashariki na kaskazini mwa nchi hiyo.

Afghanistan ambayo hivi sasa inaongozwa na serikali ya muda ya Taliban, ikiwa inakabiliwa na masaibu kadhaa, yakiwemo ya kupunguziwa misaada, vikwazo na majanga ya kimaumbile yanayojirudia, likiwemo tetemeko la ardhi la mwezi Agosti lililosababisha vifo vya watu wasiopungua 2,200, inapambana kuwapokea pia raiau milioni 4.5 ambao wamerejea nchini tangu 2023.