Uwezekano wa Marekani kuishambulia Mexico na nchi nyingine za Amerika Kusini
https://parstoday.ir/sw/news/world-i135586-uwezekano_wa_marekani_kuishambulia_mexico_na_nchi_nyingine_za_amerika_kusini
Kufuatia kuongezeka vitisho vya Rais Donald Trump dhidi ya Mexico, maafisa wa Wizara ya Vita ya Marekani wametangaza kuwa uwezekano wa kufanyika operesheni za kijeshi nchini Mexico umeongezeka.
(last modified 2026-01-17T14:51:13+00:00 )
Jan 17, 2026 09:53 UTC
  • Uwezekano wa Marekani kuishambulia Mexico na nchi nyingine za Amerika Kusini

Kufuatia kuongezeka vitisho vya Rais Donald Trump dhidi ya Mexico, maafisa wa Wizara ya Vita ya Marekani wametangaza kuwa uwezekano wa kufanyika operesheni za kijeshi nchini Mexico umeongezeka.

Kwa mujibu wa maafisa wakuu wa kijeshi wa Marekani, huenda nchi hiyo ikaendesha operesheni kubwa za kijeshi huko Mexico na nchi nyingine kadhaa za Amerika Kusini. Habari hii imechapishwa na mamlaka ya kijeshi ya Marekani, huku Rais Donald Trump, akitishia mara kwa mara kufanya operesheni za kijeshi dhidi ya Mexico. Katika siku za hivi karibuni na kufuatia uvamizi wa wa Marekani nchini Venezuela ambapo iliteka nyara na kumuondoa madarakani rais wake aliyechaguliwa kidemokrasia na watu wa nchi hiyo, Trump amekuwa akitishia mara kwa mara kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya kile anachodai ni wauzaji wa dawa za kulevya huko Mexico.

Wakati huo huo, kundi moja la Wairani wanaoishi Uholanzi limelaani uingiliaji wa kigeni katika masuala ya ndani ya Iran kwa kukusanyika mbele ya Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya nchi hii.

Katika maandamano hayo yaliyofanyika siku ya Ijumaa kwa kuhudhuriwa na idadi kubwa ya Wairani wanaoishi Uholanzi na raia kadhaa wa nchi nyingine, washiriki walipiga nara na kusoma taarifa za kulaani vikali uingiliaji wa nchi za Magharibi hususan Marekani katika masuala ya ndani ya Iran. Katika taarifa iliyosomwa katika hadhara hiyo, washiriki wamesisitiza juu ya kuunga mkono mamlaka na uhuru wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kutaka kukomeshwa uingiliaji kati na mashinikizo ya kigeni dhidi ya taifa la Iran.