Wananchi Pakistan, Iraq waandamana kuiunga mkono Iran, Kiongozi Muadhamu
https://parstoday.ir/sw/news/world-i135620-wananchi_pakistan_iraq_waandamana_kuiunga_mkono_iran_kiongozi_muadhamu
Wananchi katika nchi za Pakistani na Iraq wamefanya maandamano kuiunga mkono Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei mbele ya vitendo vya kigaidi vya hivi karibuni vilivyofadhiliwa na Marekani, Israel na madola mengine ya kibeberu.
(last modified 2026-01-18T07:04:21+00:00 )
Jan 18, 2026 07:04 UTC
  • Wananchi Pakistan, Iraq waandamana kuiunga mkono Iran, Kiongozi Muadhamu

Wananchi katika nchi za Pakistani na Iraq wamefanya maandamano kuiunga mkono Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei mbele ya vitendo vya kigaidi vya hivi karibuni vilivyofadhiliwa na Marekani, Israel na madola mengine ya kibeberu.

Televisheni ya Al Alam imetangaza kuwa, maelfu ya wananchi wa Pakistan wamefanya maandamano huko Kashmir na maeneo mengine kuonesha uungaji mkono wao kwa taifa la Iran na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu dhidi ya vitendo vya kigaidi vya hivi karibuni vilivyotokea nchini Iran.

Wananchi hao wa Pakistan wamelaani vikali kitendo cha Marekani cha kuingilia masuala ya ndani ya Iran na njama za Washington na utawala wa Kizayuni dhidi ya Iran. Aidha televisheni hiyo imetangaza kuwa, kwa siku ya pili mfululizo, wananchi wa Iraq wamemiminika kwenye mitaa ya Baghdad na miji mingine kama Mosul na Najaf, kulaani sera za kivita za Marekani dhidi ya Iran. Maandamano kama hayo yamefanyika pia katika nchi za India na Uturuki kulaani sera za kivita za Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Inafaa kuzingatia hapa kwamba hivi karibuni, kutokana na matatizo ya maisha na masuala ya kiuchumi, kulifanyika maandamano ya amani katika baadhi ya miji nchini Iran; lakini baada ya magaidi na madola ya kibeberu yakiongozwa na Marekani kuona kuwa serikali ya Iran inachukua hatua athirifu za kutatua matatizo hayo, zilimimina magenge ya kigaidi yenye silaha na yaliyopewa fedha, vifaa, mafunzo na silaha na Marekani na Israel ili kufanya mauaji na jinai nyinginezo ndani ya Iran. Magenge hayo yalibadilisha maandamano ya amani kuwa ya ghasia huku rais wa Marekani, Donald Trump akitishia mara kwa mara kuivamia kijeshi Iran. Lakini baada ya Jamhuri ya Kiislamu kuyadhibiti magenge hayo ya kigaidi na kurejesha utulivu humu nchini, Marekani imegeuza maneno na kudai haina nia ya kushambulia kijeshi Iran.