Viongozi wa Kisunni watoa wito wa msaada wa ulimwengu kwa Iran
https://parstoday.ir/sw/news/world-i138172-viongozi_wa_kisunni_watoa_wito_wa_msaada_wa_ulimwengu_kwa_iran
Wanazuoni wa Kisunni kutoka pembe zote za dunia wamehimiza umoja wa Kiislamu na kutoa wito wa kuungwa mkono kwa Iran, katika kongamano la kipekee lililofanyika Jumatatu asubuhi chini ya uratibu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu yenye makao yake Tehran.
(last modified 2026-05-05T05:39:14+00:00 )
May 05, 2026 05:34 UTC
  • Viongozi wa Kisunni watoa wito wa msaada wa ulimwengu kwa Iran

Wanazuoni wa Kisunni kutoka pembe zote za dunia wamehimiza umoja wa Kiislamu na kutoa wito wa kuungwa mkono kwa Iran, katika kongamano la kipekee lililofanyika Jumatatu asubuhi chini ya uratibu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu yenye makao yake Tehran.

Mkutano huo wa mtandaoni ulikuwa sehemu ya mfululizo wa mihadhara iliyopewa jina “Umoja Mtakatifu: Ufunguo wa Ushindi.”

Kikao hicho cha wiki hii kimejadili mmauadhui ya “Ulazima wa Waislamu Kuiunga Mkono Iran ya Kiislamu,” na kilihusisha hotuba za viongozi maarufu wa madhehebu ya Ahul Sunna, wakiwemo kutoka Iran, ambao wametoa msisitizo mkubwa juu ya nafasi ya mshikamano katika kukabiliana na vitisho vya nje na katika kuimarisha umma wa Kiislamu kwa upana wake.

Sheikh Mostafa Nouri, Imamu wa Kisunni wa Swala ya Ijumaa katika Mkoa wa Fars, Iran, amesisitiza kuwa njama za maadui wa nje zinaweza kushindwa tu kupitia umoja na mshikamano.

Amesema: “Mshikamano wa kitaifa umekuwa nguzo muhimu katika kuvuruga mipango ya wapinzani wetu. Ushirikiano kati ya nchi za Kiislamu unaweza kuimarisha zaidi umma wa Kiislamu, japo wakati mwingine msaada huo umekuwa hafifu.”

Ameongeza kuwa umoja wa kudumu na uvumilivu ni muhimu, akionesha matumaini kuwa imani, mshikamano, na uwezo wa ndani vitaiwezesha Iran kusimama imara na kufikia mustakabali wenye nguvu na ustawi.

Mamosta Iqbal Bahmani, mwakilishi wa Kisunni kutoka Mkoa wa Kurdistan, Iran katika Baraza la Wanazuoni Wataalamu Wanaochaguao Kiongozi Muadhmu, amebainisha kuwa uungaji mkono kwa Iran una misingi ya kisheria ya Kiislamu.

Amefafanua kwa kusema: “Kwa mujibu wa mafundisho ya dini, Muislamu hatakiwi kuogopa nguvu wala mali za maadui, bali lazima aamini kuwa ushindi unatokana na imani na umoja.”

Aidha amesema: “Kulinda ardhi za Kiislamu dhidi ya uvamizi wa kigeni ni jukumu la pamoja. Iwapo nchi ya Kiislamu itashambuliwa na adui, ni wajibu wa kidini kwa raia wake kujihami, na msaada kutoka kwa Waislamu wengine ni jukumu la kisharia.

Katika hali ya sasa ambapo Iran inakabiliwa na mashinikizo, tunasisitiza umuhimu wa umoja ndani ya Umma wa Kiislamu. Mafundisho ya dini yanatukataza kunyamaza mbele ya dhulma, bali twapaswa kusaidiana.”

Naye Mamosta Adel Gholami, Imamu wa Kisunni wa Swala ya Ijumaa katika eneo la Qasr-e Shirin, Iran, amegusia migogoro inayowaka katika ulimwengu wa Kiislamu – ikiwemo Palestina, Lebanon, Yemen, Syria, Iraq, na Afghanistan – akisema chanzo chake ni njama za maadui, hususan Israel na Marekani. 

Akhund Allah-Tomaj, mwanachama wa Baraza la Utamaduni wa Kisunni Iran naye amesema msaada kwa Iran una msingi katika ustaarabu wa Kiislamu wa umoja.

Amesema: “Ustaarabu wa Kiislamu ni zao la jitihada za pamoja za mataifa ya Kiislamu, na Iran imekuwa na mchango mkubwa – kuanzia taaluma, falsafa, usanifu hadi fasihi.

Kwa upande wake, Khadijeh Esmaeilpour, mwenyekiti wa Kitengo cha Wanawake na Familia katika mji wa Boukan, amesisitiza kuwa: “Iran imekuwa ikizisaidia baadhi ya nchi za Kiislamu umekuwa mkubwa hivyo umoja wa Umma wa Kiislamu unaweza kusaidia kuvuka misukosuko na changamoto zinazoukabilia ulimwengu wa Kiislamu.

Amesema siri ya mafanikio ya Mapinduzi ya Kiislamu imo katika imani, umoja, subira na ushiriki hai wa wananchi , njia ambayo inaahidi mustakabali madhubuti kwa Iran ya

Kiislamu.”