Eurasia Group: Donald Trump, hatari kubwa zaidi ya dunia mwaka 2017
https://parstoday.ir/sw/news/world-i25154-eurasia_group_donald_trump_hatari_kubwa_zaidi_ya_dunia_mwaka_2017
Taasisi ya Eurasia Group imetangaza kuwa Rais Donald Trump wa Marekani ndiyo hatari kubwa zaidi kwa usalama na amani ya dunia.
(last modified 2026-04-28T05:09:17+00:00 )
Feb 14, 2017 23:29 UTC
  • Eurasia Group: Donald Trump, hatari kubwa zaidi ya dunia mwaka 2017

Taasisi ya Eurasia Group imetangaza kuwa Rais Donald Trump wa Marekani ndiyo hatari kubwa zaidi kwa usalama na amani ya dunia.

Katika ripoti yake ya kila mwaka inayochunguza na kufanya tathmini ya hatari zinazokabili usalama na amani ya dunia iliyotolewa kwenye Mkutano wa Usalama wa Munich, taasisi ya Eurasia Group imesema kuwa, Rais wa Marekani Donald Trump ndio hatari kubwa zaidi ya usalama wa dunia. 

Uchunguzi wa taasisi hiyo unasema, Trump anachukua hatua zake kwa lengo tu la kutimiza maslahi ya Marekani bila ya kujali taathira zake mbaya kimataifa. 

Watafiti wa Eurasia Group wamesema katika ripoti hiyo kwamba, Rais Donald Trump wa Marekani ni mtu mwenye mielekeo ya upande mmoja. 

Donald Trump

Ripoti ya Eurasia Group imesema kuwa, Donald Trump anataka kudhibiti watu lakini makampuni ya teknolojia yanataka uhuru na kulindwa taarifa za watumiaji wao.

Mkutano wa Usalama wa Munich ulianza kazi zake tarehe 17 Februari ukihudhuriwa na wawakilishi wa nchi nyingi duniani ikiwemo Marekani yenyewe.