Zarif na Guterres wajadili hali ya Waislamu Warohingya nchini Myanmar
https://parstoday.ir/sw/news/world-i25336-zarif_na_guterres_wajadili_hali_ya_waislamu_warohingya_nchini_myanmar
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wamejadili na kubadilishana mawazo kuhusu hali mbaya waliyonayo Waislamu wa jamii ya Rohingya nchini Myanmar, hali ya mambo katika nchi za Yemen, Syria na Iraq na nafasi ya Umoja wa Mataifa katika kutatua migogoro hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 18, 2017 23:13 UTC
  • Zarif na Guterres wajadili hali ya Waislamu Warohingya nchini Myanmar

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wamejadili na kubadilishana mawazo kuhusu hali mbaya waliyonayo Waislamu wa jamii ya Rohingya nchini Myanmar, hali ya mambo katika nchi za Yemen, Syria na Iraq na nafasi ya Umoja wa Mataifa katika kutatua migogoro hiyo.

Katika mazungumzo aliyofanya na Katib Mkuu wa UN Antonio Guterres pembeni ya Mkutano wa Usalama wa Munich unaoendelea nchini Ujerumani, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Muhammad Javad Zarif ametaka umoja huo uwe na mchango zaidi katika kutatua migogoro inayowahusu Waislamu Warohingya wa Myamnar pamoja na hali ya mambo katika nchi za Yemen, Syria na Iraq.

Dakta Zarif ameeleza utayari wa Iran wa kushirikiana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa lengo la kutatua migogoro ya eneo.

Waislamu wa jamii ya Rohingya, Myanmar

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa UN ameashiria makubaliano ya nyuklia yaliyofikiwa baina ya Iran na nchi zinazounda kundi la 5+1 na kueleza kwamba makubaliano ya JCPOA ni wenzo muhimu wa kuimarisha amani na utahibiti kimataifa na akatangaza uungaji mkono wake na wa Umoja wa Mataifa juu ya kuendelezwa makubaliano hayo.

Antonio Guterres aidha amepokea kwa mikono miwili mwaliko aliopewa na Waziri Zarif wa kuitembelea Iran na kueleza kwamba atakapopata fursa tu atafanya safari ya kuitembelea Jamhuri ya Kiislamu ya Iran…/