Kenya yaongoza katika ununuzi wa bidhaa za Iran barani Afrika
https://parstoday.ir/sw/news/world-i29350-kenya_yaongoza_katika_ununuzi_wa_bidhaa_za_iran_barani_afrika
Kenya inaongoza katika ununuzi wa bidhaa kutoka Iran barani Afrika na ni ya 15 kwa ujumla katika ununuzi wa bidhaa za Iran duniani.
(last modified 2026-04-19T09:26:01+00:00 )
May 20, 2017 08:48 UTC
  • Kenya yaongoza katika ununuzi wa bidhaa za Iran barani Afrika

Kenya inaongoza katika ununuzi wa bidhaa kutoka Iran barani Afrika na ni ya 15 kwa ujumla katika ununuzi wa bidhaa za Iran duniani.

Kwa mujibu wa mwambata wa kibiashara wa Iran mjini Nairobi, "Kenya ni nchi ya 15 yenye kununua bidhaa kutoka Iran kwa mujibu wa takwimu za mwezi Machi mwaka 2017."

Murtadha Daylan, Mwambata wa kibiashara wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Kenya akizungumza na IRNA ameongeza kuwa, "Kenya ina umuhimu mkubwa kwa kuzingatia nchi hiyo ni mwanachama katika baadhi ya mashirika muhimu ya kibiashara ya kieneo na kimataifa kama vile Shirika la Biashara Duniani WHO, Benki ya Dunia, Jumuiya ya soko la pamoja ya Mashariki na Kusini mwa Afrika COMESA  na Jumuiya ya Afrika Mashariki."  Aidha amesema Kenya inatambulika kama lango la biashara kwa anayetaka kuingia soko la Afrika Mashariki

Murtadha Daylan ameongeza kuwa,  hatua ya serikali ya Kenya kuhimizwa ushirikiano wa kiuchumi, biashara ya kimataifa na uwekezaji nchini humo ni fursa nzuri ya kibiasahra kwa Iran.

Bendera za Kenya na Iran

Aidha amesema kwa mujibu wa mpango wa ofisi ya mwambata wa kibiashara katika Ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Nairobi katika kipindi cha mwaka moja uliopita, mashirika ya Kiirani nchini Kenya yameongezeka kutoka 10 hadi 30 katika sekta za bidhaa na huduma.

Afisa huyo wa masuala ya kibiasahra katiak ubalozi wa Iran nchini Kenya amesema kati ya mipango ya baadaye ni kuundwa chumba cha kibiashara cha pamoja baina ya Iran na Kenya kwa ajili ya kubadilishana habari na kupunguza matatizo ya kibiasahra baina ya pande mbili.