Jun 05, 2017 04:23 UTC
  • James Clapper, mkuu wa zamani wa Shirika la Kijasusi la Marekani, CIA
    James Clapper, mkuu wa zamani wa Shirika la Kijasusi la Marekani, CIA

Katika kile kinachoonekana wazi ni kuzidi kuongezeka mzozo baina ya Marekani na Russia, mkuu wa zamani wa Shirika la Kijasusi la Marekani CIA amesema kuwa, Russia ina mikakati ya muda mrefu ya kujipenyeza katika safu za viongozi wa Marekani kwa ajili ya kuwadhibiti.

James Clapper amesema hayo katika mahojiano aliyofanyiwa na televisheni ya NBC News kuhusiana na tuhuma zinazomkabili Jared Kushner, mkwe wa rais wa Marekani, Donald Trump anayedaiwa kuwa na uhusiano na Russia na kusema kwamba, hata yeye alikuwa na taarifa hizo tangu zamani na alionya kuwa Warussia wanaingilia uchaguzi wa Marekani.

Rais wa Marekani Donald Trump akipeana mkono na mkwewe, Jared Kushner

 

Mkuu wa zamani wa Shirika la Kijasusi la Marekani CIA ameongeza kuwa, kwa kawaida Russia huwa wanajiweka chini ya baadhi ya watu, kujipenyeza kwenye fikra na mambo yao na kushirikiana nao ili wawaunge mkono.

Amesema, mbinu waliyotumia Warussia katika uchaguzi uliopita nchini Marekani ilikuwa ni kueneza habari za uongo hasa kwenye mitandao ya kijamii na kuingilia moja kwa moja uchaguzi huo.

Mkuu huyo wa zamani wa CIA ameituhumu Russia kuwa inaingilia masuala ya kisiasa ya Marekani na kuitaka Washington iiwekee vikwazo Moscow.  

Tags