Wademokrat wa Marekani waanza mchakato wa kumng'oa madarakani Donald Trump
https://parstoday.ir/sw/news/world-i31228-wademokrat_wa_marekani_waanza_mchakato_wa_kumng'oa_madarakani_donald_trump
Kundi moja la Wademokrat katika Bunge la Marekani limeanzisha mchakato wa kumuuzulu Rais wa nchi hiyo, Donald Trump kutokana na mtatizo ya kiakili na kinafsi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 02, 2017 03:01 UTC
  • Wademokrat wa Marekani waanza mchakato wa kumng'oa madarakani Donald Trump

Kundi moja la Wademokrat katika Bunge la Marekani limeanzisha mchakato wa kumuuzulu Rais wa nchi hiyo, Donald Trump kutokana na mtatizo ya kiakili na kinafsi.

Kituo cha habari cha Free Beacon kimeripoti kuwa, Jamie Raskin ambaye ni mwakilishi wa chama cha Democrat katika Bunge la Marekani amewasilisha mpango ambao kwa mujibu wake itateuliwa tume maalumu itakayopewa jukumu la kuchunguza usalama wa kiakili na kinafsi wa Doland Trump. 

Wawakilishi 24 wa Bunge la Marekani akiwemo John Conyers ambaye ni mjumbe wa Kamati ya Sheria ya Congresi na Debbie Wasserman Schultz, mwenyekiti wa zamani wa Kamati ya Taifa ya chama cha Democrat, wametia saini mpango huo. 

Wamarekani wakipinga misimamo ya kibaguzi na Trump

Kwa mujibu wa katiba ya Marekani, rais wa nchi anapaswa kuuzuliwa na kuondolewa madarakani pale itakapothibitika kwamba, si mzima kinafsi na kisaikolojia kwa ajili ya kutekeleza majukumu yake. 

Katika miezi ya hivi karibuni wataalamu wa elimu nafsi na saikolojia na makundi ya wasomi wa vyuo vikuu nchini Marekani wamekuwa wakitahadharisha kuhusu mienendo na matamshi yanayotolewa mara kwa mara na rais wa nchi hiyo, Donald Trump.