Jul 11, 2017 08:14 UTC
  • Russia yawatimua wanadiplomasia 30 wa Marekani

Serikali ya Russia katika kujibu hatua ya Marekani ya mwezi Disemba mwaka jana 2016 ya kuwatimua wanadiplomasia wake 35, imewatimua wanadiplomasia 30 wa nchi hiyo kutoka nchi hiyo.

Afisa mmoja wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Russia sambamba na kukosoa kitendo cha serikali ya Marekani ya kukataa kutatua tofauti za kidiplomasia hususan katika maeneo ya Washington na New York, Moscow nayo imeamua kuchukua hatua ya kujibu hatua hiyo ya Marekani ya mwishoni mwa mwaka jana. Katika hatua hiyo Moscow imewataka wanadiplomasia 30 wa Marekani kuondoka Russia mara moja. Hatua hiyo imekuja zikiwa zimepita siku chache tangu kufanyika kikao cha Rais Vladmir Putin wa Russia na Rais Donald Trump wa Marekani huko mjini Hamburg, Ujerumani.

Marais wa Marekani na Russia walipokutana hivi karibuni Ujerumani

Katika kikao cha marais hao, kulitolewa taarifa ya pamoja kwamba pande mbili zina matumaini ya kupigwa hatua moja mbele kwa ajili ya kuboresha mahusiano yao yaliyoharibika. Disemba mwaka jana Barack Obama rais wa zamani wa Marekani alitoa amri ya kushangaza ya kuwatimua wanadiplomasia 35 wa Russia katika majengo ya kidiplomasia mjini Washington na New York. Obama alichukua hatua hiyo kwa kile alichodai kuwa ni kujibu uingiliaji wa Moscow katika masuala ya ndani ya nchi hiyo hususan katika uchaguzi mkuu uliopita.  

Tags