Wananchi wa Uingereza: Tutaandamana dhidi ya Trump
https://parstoday.ir/sw/news/world-i43708-wananchi_wa_uingereza_tutaandamana_dhidi_ya_trump
Makumi ya maelfu ya wananchi wa Uingereza wametangaza kuwa wapo tayari kushiriki katika maandamano dhidi ya ziara ya Rais Donald Trump wa Mareani mjini London.
(last modified 2025-10-23T11:19:28+00:00 )
Apr 27, 2018 08:04 UTC
  • Wananchi wa Uingereza: Tutaandamana dhidi ya Trump

Makumi ya maelfu ya wananchi wa Uingereza wametangaza kuwa wapo tayari kushiriki katika maandamano dhidi ya ziara ya Rais Donald Trump wa Mareani mjini London.

Harakati ya Civil Campaign ambayo ni miongoni mwa taasisi kubwa zinazopinga ziara ya Rais Donald Trump mjini London, Uingereza imetuma ujumbe katika ukurasa wake wa Facebook ukieleza kuwa maandamano makubwa yatafanywa mbele ya ofisi ya Waziri Mkuu wa Uingereza sambamba na safari hiyo ya Trump mjini London.   

Kwa mujibu wa takwimu zilizochapishwa katika ukurasa wa Facebook wa taasisi hiyo ya kiraia, hadi kufikia sasa zaidi ya watu elfu 85 wametangaza kuwa wapo tayari kushiriki katika maandamano dhidi ya Trump.

Rais Donald Trump wa Marekani 

Wakati huo huo taasisi mbalimbali za kiraia za nchini Uingereza pia zimewatolea wito wananchi kote nchini humo kushiriki katika maandamano hayo ya kupinga safari ya safari ya Rais wa Marekani mjini London. Wanaharakati wengine wanaopinga vita nchini Uingereza nao wamekaribisha kupingwa ziara hiyo ya Trump nchini humo inayotarajiwa kufanywa tarehe 16 Julai mwaka huu.