Kuhamishiwa wahajiri katika jela zenye ulinzi mkali huko Marekani
Televisheni ya CNN imefichua kuwa wahajiri nchini Marekani wamehamishiwa katika jela zenye ulinzi mkali.
CNN imeripoti kuwa hali ya wahajiri hao ambao walikamatwa ikiwa ni katika kutekeleza siasa za serikali za Rais Donald Trump wa Marekani za kutokuwa na uvumilivu katika kukabiliana na wahajiri haramu ni mbaya sasna huku baadhi ya wafungwa wakihamishiwa katika jela zenye ulinzi mkali huko kusini mwa California.
Televisheni ya CNN huku ikitegemea uchunguzi wa kina kutoka kwa mawakili wa Jumuiya ya Uhuru ya raia wa Marekani (ACLU) imeongeza kuwa: Wahajiri wambao wameingia kinyume cha sheria nchini Marekani wanaishi katika maisha sawa na ya jela huku wakishindwa kuwa na mawakili na kuwasiliana na ulimwengu wa nje.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo wahajiri haramu tayari wamehamishiwa katika jela zenye ulinzi mkali huko kusini mwa California. Wakati huo huo imebainika kuwa baadhi wa wahajiri pia wanashikiliwa katika jela ya shirikisho katika jimbo la Oregan huku wakiishi katika mazingira yasiyo ya kibinadamu ambapo haki za binadamu hazifuatwi. Miamala isiyo ya kibinadamu inayotekelezwa na serikali ya Marekani dhidi ya wahajiri khususan watoto wa wahajiri hao imekosolewa pakubwa ndani na nje ya nchi hiyo.
Itakukumbukwa kuwa Rais Trump wa Marekani amechukua hatua kadhaa kinzani ambapo ameamuru kusimamishwa mchakato wa kuwatenganisha watoto na familia zao za wahajiri katika mpaka wa Mexico na nchi hiyo, na wakati huo huo ameamrisha kuendelea kushikiliwa familia hizo za wahajiri kwa muda usiojulikana na ametaka kuhuhukumiwa watu hao kwa hatua yao ya kuingia Marekani kinyume cha sheria.