Sep 16, 2018 01:12 UTC
  • John Kerry ajibu mashambulizi ya kimaneno ya Trump kuhusu JCPOA

Waziri wa Mambo ya Nje wa zamani wa Marekani sambamba na kutetea mapatano ya nyuklia ya Iran maarufu kama Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji, JCPOA, amekiri kwamba, kwa kuzingatia ukiukaji wa ahadi wa Marekani, hakutofanyika mazungumzo yoyote kati ya Iran na Washington.

John Kerry ameyasema hayo akijibu matamshi ya hivi karibuni ya Rais Donald Trump wa Marekani kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter kuhusiana na mapatano hayo ambapo ameandika: "Muheshimiwa rais, ikiwa unataka mapatano ya nyuklia ambayo yaliifanya dunia kuwa ya amani zaidi, jifunze kitu kimoja kwa kununua kitabu cha Every Day Is Extra." Akiashiria kashfa nyingi ambazo zimeizingira serikali ya hivi sasa ya Washington na Rais Donald Trump, amemuusia rais huyo kwamba, ni bora ashughulishwe na wasi wasi wa kukutana na Paul Manafort, kiongozi wa zamani wa idara ya kuendesha kampeni za uchaguzi wa mwaka 2016 na Robert Mueller, mpelelezi maalumu wa faili la mahusiano ya uingiliaji wa Russia katika ushindi wa Trump.

Rais Donald Trump wa Marekani ambaye anaendelea kukosolewa kila upande

Ijumaa iliyopita Paul Manafort alikiri mahakamani mjini Washington juu ya ukiukaji wake wa kanuni za uchaguzi na kusema kuwa anashirikiana na timu ya Mueller katika uwanja huo. Hivi karibuni waziri huyo wa zamani wa mambo ya nje wa Marekani kwa mara nyingine tena alikosoa misimamo ya serikali ya rais wa hivi sasa wa nchi hiyo Donald Trump dhidi ya Iran na kuionya Ikulu ya nchi hiyo kuhusu matokeo mabaya ya siasa zake.

Tags