Uturuki yaitaka Venezuela kufanya biashara kwa kutumia sarafu za ndani
(last modified Mon, 24 Sep 2018 02:57:05 GMT )
Sep 24, 2018 02:57 UTC
  • Uturuki yaitaka Venezuela kufanya biashara kwa kutumia sarafu za ndani

Uturuki imeialika Venezuela kutumia sarafu za nchi zao badala ya dola katika miamala ya kibiashara ya pande mbili; ikiwa ni katika kampeni ya kuimarisha uchumi wa nchi hizo kukabiliana na mashinikizo ya serikali ya rais wa Marekani, Donald Trump.

 Akizungumza na waandishi wa habari akiwa na mwenzake wa Venezuela Jorge Arreaza, Mevlut Cavusoglu Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki amesema kama ninavyomnukuu: "Tuna hamu kubwa ya kutumia sarafu za nchi zetu katika biashara ya pande mbili si tu kati ya Uturuki na Venezuela bali pia kati ya Uturuki na nchi nyingine," mwisho wa kunukuu.  

Rais Donald Trump wa Marekani 

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki ameongeza kuwa mara nyingi tumekuwa tukijaribu kutumia pesa za nchi zetu katika miamala ya kibiashara kwa kuzingatia kuwa serikali ya Marekani imekuwa ikitumia sarafu ya dola kama wenzo wa kuzikandamiza nchi nyingine. Vile vile ameituhumu serikali ya Marekani kwa kutumia dola kama wenzo wa kushambulia uchumi wa nchi nyingine. Amesema Uturuki imekumbwa na matatizo ya kupanda na kushuka thamani kwa sarafu yake kutokana na kushambuliwa hivi karibuni uchumi wa nchi hiyo na serikali ya Marekani.

Kwa upande wake Jorge Arreaza, Waziri wa Mambo ya Nje wa Venezuela ameashiria uhusiano wa kidugu uliopo kati ya nchi yake na Uturuki na kubainisha kuwa Uturuki ina ushirikiano mzuri na Venezuela hasa wakati wa shida.

 

Tags