UN yataka kuzidishwa misaada kwa wahajiri
https://parstoday.ir/sw/news/world-i50029-un_yataka_kuzidishwa_misaada_kwa_wahajiri
Kamisheni Kuu ya Wakimbizi ya Umoja wa Mataifa imeeleza wasiwasi wake mkubwa kuhusu hatua ya kusitishwa operesheni ya uokoaji ya meli ya Aquarius na kutoa wito wa kuzidishwa misaada ya kuokoa wahajiri katika Bahari ya Mediterania.
(last modified 2026-02-22T02:21:18+00:00 )
Dec 08, 2018 08:16 UTC
  • UN yataka kuzidishwa misaada kwa wahajiri

Kamisheni Kuu ya Wakimbizi ya Umoja wa Mataifa imeeleza wasiwasi wake mkubwa kuhusu hatua ya kusitishwa operesheni ya uokoaji ya meli ya Aquarius na kutoa wito wa kuzidishwa misaada ya kuokoa wahajiri katika Bahari ya Mediterania.

Msemaji wa Kamisheni Kuu ya Wakimbizi ya Umoja wa Mataifa, Shabia Mantoo amesema kuwa, kuna udharura wa kuzidishwa operesheni za kuokoa wahajiri katika Bahari ya Mediterania na si kupunguza operesheni hizo.

Ravina Shamdasani ambaye pia ni msemaji wa Kamisheni Kuu ya Wakimbizi ya Umoja wa Mataifa amesema ni suala lisilokubalika kutambua operesheni za kuokoa na kuwasaidia wahajiri kuwa ni uhalifu na kosa la jinai. Ameyasema hayo baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani wa Italia, Matteo Salvini kuzituhumu jumuiya za misaada ya kibinadamu zinazowasaidia wahajiri kuwa zinashirikiana na wahalifu wa magendo ya binadamu huko Libya.

Vilevile jumuiya za kutetea haki za binadamu zimelaumu hatua ya simamishwa operesheni za meli ya Aquarius za kuokoa wahajiri katika maji ya Bahari ya Mediterania.

Meli hiyo ilikuwa ikiokoa wahajiri kutoka nchi mbalimbali na kuwapeleka barani ulaya. 

Wahajiri wa Kiafrika wakwia baharini.

Nchi nyingi za Ulaya zimeipiga marufu meli hiyo kuokoa wahajiri wanaozama katika Bahari ya Mediterania na kuwapeleka katika nchi hizo. Tangu mwezi Februari mwaka 2016 hadi sasa meli ya Aquarius imeokoa na kusaidia wahajiri elfu 30.  

Maelfu ya wahajiri wamefariki dunia katika bahari hiyo wakiwa katika pirikapirika za kuelekea Ulaya kutafuta maisha bora.