Jeshi la Venezuela lapiga gwaride la kumuunga mkono Rais Maduro
(last modified Mon, 28 Jan 2019 08:24:18 GMT )
Jan 28, 2019 08:24 UTC
  • Jeshi la Venezuela lapiga gwaride la kumuunga mkono Rais Maduro

Jeshi la Venezuela limepiga gwaride mbele ya Rais Nicolás Maduro wa nchi hiyo likitangaza kumuunga mkono.

Katika gwaride hilo Rais Maduro akiwa kando na Vladimir Padrino López, Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo amesema kuwa maonyesho hayo ya kijeshi yameuthibitishia ulimwengu kwamba, serikali ya Caracas inaungwa mkono na jeshi. Aidha ameongeza kwamba hakuna mtu anayewaunga mkono watu dhaifu, waoga na mahaini. Rais Nicolás Maduro amesema kuwa gwaride hilo limefanyika katika hali ambayo kila siku maelfu ya jumbe kupitia mitandao ya kijamii kutoka Colombia zinatumwa kwenda kwa askari wa serikali ya Venezuela zikiwataka wajiunge na wapinzani. Sambamba na kufanyika maonyesho hayo ya kijeshi katika kumuunga mkono Rais Maduro, raia waungaji mkono wake pia wameanzisha kampeni katika mitandao ya kijamii yenye ujumbe unaosema: "Daima Utiifu, na Kamwe Uhaini."

Rais Nicolás Maduro wa Venezuela

Jeshi hilo limetangaza uungaji na utiifu wake kwa Rais Nicolás Maduro katika hali ambayo Juan Guaidó amewataka askari kujiunga naye. Wakati huo huo hatua ya viongozi wa serikali ya Venezuela kuonyesha picha za kiongozi wa wapinzani akipanga njama dhidi ya serikali, imemzidishia kashfa kiongozi huyo. Jana George Rodriguez's, Makamu wa Rais katika Masuala ya Mawasiliano, Utamaduni na Utalii wa Venezuela, alionyesha mkanda wa video unaoonyesha uhaini wa Juan Guaidó na baadhi ya viongozo wengine wa upinzani.

Tags