Afisa wa CIA: Adel al-Jubeir ana mawasiliano makubwa na MOSSAD
(last modified Mon, 18 Feb 2019 14:34:19 GMT )
Feb 18, 2019 14:34 UTC
  • Afisa wa CIA: Adel al-Jubeir ana mawasiliano makubwa na MOSSAD

Afisa wa zamani wa Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA) amefichua kwamba Adel al-Jubeir, Waziri wa Masuala ya Nje wa Saudia ana mawasiliano ya karibu na Shirika la Kijasusi la Utawala wa Kizayuni wa Israel, MOSSAD.

Kwa mujibu wa Philip Giraldi, al-Jubeir alitambulishwa na mmoja wa marafiki wake anayejulikana kwa jina la Ken Matthews kufanya biashara na kukutana na viongozi wakubwa wa utawala wa Kizayuni. Giraldi amesema kuwa wakati alipohojiwa na polisi ya Federali ya Marekani FBI, mwezi Agosti 1998 Adel al-Jubeir alikiri kukutana na mmoja wa majasusi wakubwa wa MOSSAD hapo mwaka 1995. Amezidi kufafanua kuwa, katika kufungamana kibiashara na viongozi wa Israel, hatimaye al-Jubeir alianza kushirikiana na shirika hilo la Kizayuni.

Philip Giraldi, Afisa wa zamani wa Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA)

Inaelezwa kuwa wakati huo Ken Matthews alitoa amri kwa shirika hilo kukata mawasiliano na al-Jubeir. Aidha Philip Giraldi amepanga kufichua zaidi katika kitabu chake kuhusu maisha ya Adel al-Jubeir namna alivyopanda ngazi kutoka msemaji wa ubalozi na kuwa balozi kamili wa Saudia nchini Marekani na kisha kutoka hapo akawa Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo. Katika kitabu hicho, afisa wa zamani wa Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA) atafichua ushirikiano mkubwa uliopo baina ya MOSAAD na al-Jubeir hadi sasa. Ufichuaji huo unajiri katika hali ambayo viongozi wa utawala wa Aal-Saud akiwemo Mohammad Bin Salman, Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa Saudia ni kati ya watu wenye uhusiano wa karibu zaidi na utawala haramu wa Kizayuni.

Tags