Lavrov: Matamshi ya Bolton dhidi ya Venezuela ni ya udhalilishaji
(last modified Tue, 05 Mar 2019 02:43:59 GMT )
Mar 05, 2019 02:43 UTC
  • Lavrov: Matamshi ya Bolton dhidi ya Venezuela ni ya udhalilishaji

Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia ameyataja matamshi yaliyotolewa na Mshauri wa Usalama wa Taifa wa Marekani dhidi ya Venezuela kuwa ni udhalilishaji kwa Amerika ya Latini.

Sergei Lavrov ameashiria matamshi hayo ya John Bolton aliyesema kuwa  Washington inaitazama Venezuela kwa mujibu wa doktrini ya James Monroe na kuongeza kuwa matamshi hayo yanazidhalilishaji nchi zote za Amerika ya Latini. Lavrov ameongeza kuwa huko nyuma pia viongozi wa Marekani walitoa matamshi ya vitisho ambapo walisema kuwa Venezuela si mwisho wa mchezo na kwamba Cuba na Nicaragua ndizo zitakazofuata.  

Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amesema nchi zalendo za Amerika ya Latini zinapasa kuonyesha radiamali kwa matamshi hayo ya Bolton. Siku kadhaa zilizopita alikitaja kile alichosema ni doktrini ya Monroe na kudai kuwa Washington ina haki ya kuingilia masuala ya nchi za Amerika ya Latini. Doktrini ya Monroe kwa mara ya kwanza iliasisiwa katika karne ya 19 ya rais wa wakati huo wa Marekani James Monroe kwa lengo la kukabiliana na kupanuka mapigano ya wakoloni wa Ulaya katika bara la Amerika. 

John Bolton, Mshauri wa Usalama wa Taifa wa Marekani
 

Hata hivyo doktrini hiyo imebadilishwa katika miongo ya karibuni kwa visingizio vya Marekani ili kuiwezesha nchi hiyo kuinglia masuala ya ndani ya nchi jirani lengo likiwa ni kuhalalisha kuingia madarakani serikali inazozitaka. 

Tags