Hatua mpya ya Rais Maduro kufanya mabadiliko katika serikali ya Venezuela
(last modified Tue, 19 Mar 2019 08:09:23 GMT )
Mar 19, 2019 08:09 UTC
  • Hatua mpya ya Rais Maduro kufanya mabadiliko katika serikali ya Venezuela

Wakati mgogoro wa kisiasa nchini Venezuela ukiwa unaendelea hasa "Vita vya Umeme" na huku kinara wa upinzani Juan Guaido hakiwa ameshahidisha uchochezi wake baada ya kujitangaza kuwa rais kwa lengo la kuidhoofisha serikalii halali, Rais Nicholas Maduro ambeye ni rais halali wa nchi hiyuo imechukua hatua za kuleta uthabiti na kuimarisha serikali ya nchi hiyo.

Kuhusiana na hili, Rais Maduro amewataka mawaziri wote wajiuzulu ili aunde baraza la mawaziri lenye uwezo wa kuenda kazi vizuri zaidi.

Delcy Rodriguez Makamu wa Rais wa Venezuela katika ujumbe kupitia Twitter alitangaza kuwa: "Maduro amewataka mawaziri wote wajiuzulu ili kuimarisha serikali na pia kuilinda ardhi ya nchi hiyo na kuiwezesha kukabiliana na kila aina ya vitisho."

Mabadiliko  haya yanafanyika baada ya wiki moja ya kukatika umeme Venezuela na hivyo kupelekea nchi hiyo yenye utajiri mkubwa wa mafuta ya petroli kutumbukia katika kiza.

Katika upande mwingine Venezuela inakabiliwa na uporomokaji wa uchumi wake kutokana na mfumo mkubwa sana wa bei, ukosefu wa bidhaa muhimu za chakula na dawa na pia idadi kubwa ya watu kuihama nchi hiyo.

Maduro anasema ushahidi unaonyesha kuwa kukatika umeme nchini humo kumetokana na hujuma ya Marekani na mtandao wa kompyuta nchini humo katika vituo vya umeme. Amesema Marekani inashirikiana na waharibifu wa ndani ya nchi katika kuhujumu vituo vya kusambaza umeme nchini humo.

Wiki iliyopita Rais Maduro aliwahutubia wananchi katika mji mkuu Caracas, na kusema Marekani imeanzisha "Vita vya Umeme" dhidi ya nchi yake na kusema kukatika umeme nchini humo kumetokana na na hujuma ya kimtandao ya madola ya kibeberu.

Mnamo Januari 23, baada ya kufanyika sherehe ya kuapishwa Maduro kama rais aliyechaguliwa kwa wingi wa kura za wananchi, Juan Guaido kiongozi wa upinzani alijitangaza kuwa rais.

Kinara wa upinzani Venezuela  Juan Guaido  

Nchi kama vile Canada na Marekani na baadhi ya nchi waitifaki wao zilimtambua kinara huyo wa upinzani kama rais.

Hii ni katika hali ambayo, Russia, China, Mexico, Cuba, Nicaragua, Bolivia, Uturuki, Iran, Serbia, Syria, Afrika Kusini na nchi zingine nyingi duniani zimetangaza kumuunga mkono Maduro kama rais halali wa Venezuelana na zimetaka madola makubwa yaache kuingilia mambo ya ndani ya nchi hiyo ya Amerika ya Latini.

Katika hali ambayo aghalabu ya nchi duniani zinaunga mkono urais wa Maduro nchini Venezuela, lakini Marekani na waitifaki wake wanafuatilia sera ya vitisho dhidi ya nchi zingine ambazo wanazilazimisha zisimtambue Maduro. Serikali ya Trump imeshadidisha vikwazo dhidi ya Venezuela kwa lengo la kuidhoofisha serikali ya nchi hiyo na kuyafanya masiha ya wananchi yawe magumu ili waache kuingia mkono serikali halali.

Elliot Abrams, mjumbe maalumu wa serikali ya Marekani katika masuala ya Venezuela, manamo 12 Machi alisema katika mkutano na waandishi habari kuwa: "Sisi tutazidisha vikwazo dhidi ya Venezuela katika siku zijazo, vikiwemo vikwazo vipya dhidi ya taasisi za kifedha ambazo zinafanya kazi na Venezuela."

Katika wiki za hivi karibuni Marekani imezidisha mashinikizo yake dhidi ya serikali ya Venezuela ili kumlazimi Nicholas Maduro aondoke madarakani na mahala pake pachukuliwe na Juan Guaido  ambaye amejitangaza rais kinyume cha sheria.

Rais wa Venezuela akiwa mbele ya wananchi

Pamoja na kuwepo njama hiyo, Maduro amesisitiza mara kadhaa kuwa hatasalimu amri mbele ya mashinikizo ya Marekani na vibaraka wake  na hivyo hataondoka katika nafasi yake ya kisheria ya urais wa Venezuela.

Umoja wa Mataifa umepinga vikali jaribio lolote la uingiliaji wa kijeshi Venezuela na kusisitiza kuhusu utatuzi wa kisiasa wa mgogoro wa nchi hiyo kupitia mazungumzo.

Kwa mtazamo wa nchi ambazo zinapinga uingiliaji kijeshi wa Marekani Venezuela kama vile Russia, Marekani inalenga kuiangusha serikali ya Venezuela haraka ili hiyo iwe hatua ya mwanzao katika kuziangusha serikali zingien za mrengo wa kulia Amerika ya Latini hsa Nicaragua, Cuba na Bolivia.

Tags