Wafanyakazi Indonesia wapewa mshahara maradufu Ramadhani
https://parstoday.ir/sw/news/world-i53430-wafanyakazi_indonesia_wapewa_mshahara_maradufu_ramadhani
Wafanyakazi nchini Indonesia wanatazamia kupewa mshahara mara mbili katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani, ili kuwawezesha kufurahia sikukuu ya Idul Fitr ambayo ni moja ya likizo ndefu zaidi nchini humo.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
May 12, 2019 07:39 UTC
  • Wafanyakazi Indonesia wapewa mshahara maradufu Ramadhani

Wafanyakazi nchini Indonesia wanatazamia kupewa mshahara mara mbili katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani, ili kuwawezesha kufurahia sikukuu ya Idul Fitr ambayo ni moja ya likizo ndefu zaidi nchini humo.

Mshahara huo maradufu hutolewa nchini Indonesia chini ya Sheria ya 'Marupurupu ya Likizo za Kidini' (THR).

Kila mwaka unapofika mwezi wa Ramadhani nchini Indonesia, wafanyakazi rasmi hulipwa mshahara mara mbili ili kuwawezesha wao na familia zao kufurahia mwezi huo sambamba na kujiandaa kwa ajili ya sherehe za Idi.

Aidha wafanyakazi ambao sio waumini wa dini tukufu ya Uislamu hupewa nyongeza hiyo katika misimu yao ya kidini.

Waislamu nchini Indonesia

Indonesia ni nchi yenye idadi ya watu wapatao milioni 264, ambapo asilimia 87 ya wakaazi wa nchi hiyo ni Waislamu.

Asilimia 10 ya jamii ya Waindonesia ni Wakristo, asilimia 1.7 ni Wahindu huku asilimia 1.3 ya watu wa nchi hiyo ikijengwa na wafuasi wa dini nyinginezo.