Marekani yajaribu kufanya tena mazungumzo na Korea ya Kaskazini
(last modified Mon, 02 Sep 2019 04:06:31 GMT )
Sep 02, 2019 04:06 UTC
  • Marekani yajaribu kufanya tena mazungumzo na Korea ya Kaskazini

Viongozi wa Marekani wanajaribu kila linalowezekana kufanya tena mazungumzo na Korea ya Kaskazini kufuatia tahadhari iliyotolewa na serikali ya Pyongyang.

Afisa katika Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Marekani bila ya kutoa maelezo yoyote amesema kuwa Washington iko tayari kufanya mazungumzo na Korea ya Kaskazini haraka iwezekanavyo mara tu nchi hiyo itakapokuwa tayari. Korea ya Kaskazini imeitahadharisha Washington kwamba Pyongang imeanza kupoteza matarajio yake taratibu kuhusu kufanya mazungumzo na Marekani. 

Choe Son Hui Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea ya Kaskazini ameeleza kuwa matamshi na misimamo ya Mike Pompeo Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani kuhusu Pyongyang inalifanya suala la mazungumzo kati ya nchi mbili hizo kuwa gumu zaidi. Pompeo Alhamisi iliyopita alidai kuwa sera za kutojali za Korea ya Kaskazini haziwezi kufumbiwa macho.

Choe son Hui, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea ya Kaskazini 
 

Mazungumzo kati ya Marekani na Korea ya Kaskazini kuhusu masuala ya nyuklia ya Peninsula ya Korea yamesitishwa tangu viongozi wa nchi mbili hizo wakutane huko Hanoi mji mkuu wa Vietnam mwezi Februari mwaka huu. 

Tags