Novak: Russia kuwekeza zaidi katika sekta ya mafuta ya Iran
Waziri wa Nishati wa Russia amesema kuwa nchi yake inachunguza uwezekano wa kuwekeza zaidi katika uzalishaji wa mafuta nchini Iran.
Akitoa maelezo zaidi kuhusu uwekezaji wa nchi hiyo katika sketa ya mafuta hapa nchini, Alexander Novak amesema kuwa suala la kwanza katika uwanja huo litahusu uchimbaji mafuta. Waziri wa Nishati wa Russia alibainisha hayo jana pambizoni mwa Mkutano wa 5 wa Uchumi wa Mashariki uliofanyika katika mji wa Vladivostok nchini Russia.
Kabla ya hapo pia, Sergei Ryabakob Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia alisema kuwa nchi yake iko tayari kushirikiana na Iran katika nyanja za mafuta na fedha. Alisisitiza kuwa Iran sasa inapasa kuuza nje kiwango cha mafuta kulinganisha ni kile ilichouza kabla ya Mei mwaka jana. Mkutano wa Tano wa Uchumi wa Kimataifa wa Mashariki ambao ulianza juzi katika mji wa Vladivostok Russia kwa kuhudhuriwa na wawakilishi kutoka makumi ya nchi duniani unaendelea hadi leo.