Russia: Vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran vimefeli
https://parstoday.ir/sw/news/world-i57128-russia_vikwazo_vya_marekani_dhidi_ya_iran_vimefeli
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amesema kuwa, vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran havina natija yoyote na vimefeli.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 08, 2019 04:32 UTC
  • Russia: Vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran vimefeli

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amesema kuwa, vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran havina natija yoyote na vimefeli.

Sergei Ryabkov aliyasema hayo jana ambapo sambamba na kukosoa vikwazo vipya vya upande mmoja vya Marekani dhidi ya Iran, ameongeza kuwa, mwenendo huo umefeli na hauna maslahi yoyote kwa siasa za kigeni za Washington. Ryabkov ameongeza kwamba vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran na nchi nyingine za dunia, si halali na ni wenzo unaotumiwa na Washington kuzitwisha nchi nyingine matakwa yake. Mwezi Mei mwaka jana serikali ya Marekani sambamba na kujiondoa kwenye mapatano ya nyuklia ya JCPOA iliiwekea vikwazo vikali serikali ya Iran kuanzia sekta ya mafuta, benki na shughuli za maendeleo.

Sergei Ryabkov, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia.

Katika radiamali yake na kwa kutegemea vifungu viwili vya mapatano hayo, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iliamua kupunguza hatua kwa hatua uwajibikaji wake kwenye mapatano hayo ambapo Jumatano iliyopita ilianza kutekeleza hatua ya nne ya kupunguza uwajibikaji huo. Kuhusiana na suala hilo, televisheni ya Bloomberg ya nchini Marekani hivi karibuni ilitoa ripoti ikisema kuwa, siasa za Washington dhidi ya Iran zimefeli na kwamba hivi sasa Marekani haina chaguo jingine la kuiwekea vikwazo zaidi nchi hii.