May 14, 2020 03:51 UTC
  • Rais Tayyip Erdoğan: Lobi za Kiarmania ni 'wafuasi wa shetani'

Katika hotuba yake ya hivi karibuni aliyoitoa kupitia televisheni, Rais Recep Tayyip Erdoğan wa Uturuki amezitaja lobi za Kiarmenia kuwa ni 'wafuasi wa shetani.'

Kwa mujibu wa rais huyo, hivi sasa lobi hizo zinaiandama Uturuki. Katika hotuba hiyo aliyoitoa kuhusiana na mazingira ya sasa katika eneo sambamba na kuenea kwa virusi vya Corona Erdogan ameongeza kuwa, Uturuki itaendeleza mapambano yake dhidi ya ugaidi na adui yeyote wa nje wakiwemo wale aliowataja kuwa wanachama wa shetani. Rais huyo wa Uturuki amesema watu hao aliowaita kuwa ni wafuasi wa shetani kwamba ni pamoja na lobi za Kiarmania na Ugiriki.

Viongozi wa Uturuki na Marekani ambao wamekuwa wakivutana kuhusiana na kadhia ya mauaji ya Waarmenia

Rais Recep Tayyip Erdoğan amesema tena kwamba baadhi ya wapinzani wa serikali yake wanapata fedha kutoka taasisi za kifedha za kigeni ili waiwekee vizuizi serikali ya Uturuki. Marekani na Uturuki zimekuwa na mvutano mkubwa kuhusiana na suala la mauaji makubwa yaliyofanywa dhidi ya Waarmenia, ambapo Washington inaituhumu Uturuki kuhusika na jinai hiyo, huku kwa upande wake serikali ya Ankara ikitupilia mbali tuhuma hizo.

Tags