Waislamu waandamana Paris kulaani vitendo vya uchupaji mipaka
(last modified Sun, 25 Oct 2020 03:11:09 GMT )
Oct 25, 2020 03:11 UTC
  • Waislamu waandamana Paris kulaani vitendo vya uchupaji mipaka

Waislamu kadhaa wanaoishi nchini Ufaransa wamefanya maandamano katika mji mkuu wa nchi hiyo Paris lengo likiwa ni kulaani vitendo vya ghasia na uchupaji mipaka.

Waislamu hao wakazi wa Paris wameandamana kuelekea katika shule moja katika mji mkuu huo ambayo mwalimu  Profesa Samuel Paty alikuwa akifundisha. Mwalimu huyo ameuawa hivi karibuni katika shambulio la mtu aliyekuwa na silaha baridi. 

Mwalimu Samuel Paty aliyeuawa kwa silaha baridi huko Paris 

Waislamu sawa kabisa na jamii nyingine ya raia wanaoishi nchini Ufaransa wamelaani pakubwa mauaji ya mwalimu huyo Mfaransa. Polisi ya Ufaransa Ijumaa iliyopita ilitangaza kuwa kijana mmoja wa miaka 18 raia wa Chechniya alimshambulia na kumuuwa kwa silaha baridi mwalimu mmoja huko Paris. Profesa Samuel Paty aliwahi kuwaonyesha wanafunzi wake picha za vibonzo vya kumvunjia heshima Mtume Mtukufu wa Uislamu(S.A.W).  

Serikali ya Ufaransa imefunga msikiti mmoja huko Paris na kuchukua uamuzi wa kuwafukuza nchini humo raia 231 wa kigeni  kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya kufurutu ada baada ya kukamatwa watu watano kuhusiana na mauaji hayo.Weledi wa mambo kwa upande wao wanaamini kuwa Paris inatumia tukio hilo ili kutekeleza sera zake dhidi ya Uislamu.