Makumbusho kubwa ya Muhammadiyah kufunguliwa nchini Indonesia mapema 2021
https://parstoday.ir/sw/news/world-i64780-makumbusho_kubwa_ya_muhammadiyah_kufunguliwa_nchini_indonesia_mapema_2021
Makumbusho ya Muhammadiyah iliyojengwa katika mji mkuu wa Indonesia Jakarta inatazamiwa kuwa makumbusho kubwa kabisa kuhusu Bwana Mtume Muhammad SAW.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Nov 22, 2020 12:33 UTC
  • Makumbusho kubwa ya Muhammadiyah kufunguliwa nchini Indonesia mapema 2021

Makumbusho ya Muhammadiyah iliyojengwa katika mji mkuu wa Indonesia Jakarta inatazamiwa kuwa makumbusho kubwa kabisa kuhusu Bwana Mtume Muhammad SAW.

Ripoti ya shirika la habari la FARS imeeleza kuwa, ujenzi wa makumbusho hiyo ya Muhammadiyah umekamilika na ufunguzi wake rasmi utafanyika Februari 2021 na hivyo kuifanya makumbusho kubwa zaidi yenye athari zinazomhusu Mtume SAW.

Mkurugenzi wa makumbusho hiyo Kurnayavan ameeleza kwamba, anatumai kujengwa kwa makumbusho hiyo kutaweza kusaidia kumtambulisha Bwana Mtume Muhammad SAW na kumfanya afahamike zaidi kwa kizazi kipya cha vijana wa Indonesia.

Indonesia ni nchi iliyoko kusini mashariki ya Asia na ina idadi ya watu milini 273, ambapo asilimia 86 miongoni mwao ni Waislamu, jambo ambalo limeifanya nchi hiyo iupe umuhimu mkubwa utamaduni na mtindo wa maisha wa Kiislamu.../