Nov 29, 2020 01:31 UTC
  • Mwanajeshi wa Marekani atiwa mbaroni kwa kushirikiana na magaidi wa Syria

Mahakama moja ya jimbo la New Jersy la nchini Marekani imetoa amri ya kutiwa mbaroni mwanajeshi mmoja wa nchi hiyo kwa tuhuma za kushirikiana na genge la kigaidi la Tahrir al Sham lililobadilisha jina na kujiita Jabhat al Nusra nchini Syria.

Hayo yameripotiwa na mtandao wa The Hill na kuongeza kuwa, Maria Bell, (53) mwanajeshi mtaafu wa Marekani anashtakiwa kwa makosa ya kumsaidia kifedha mwanachama mmoja wa genge la kigaidi la Tahrir al Sham au Jabhat al Nusra nchini Syria.

Sehemu moja ya mashtaka yanayomkabili mwanajeshi huyo wa zamani wa Marekani inasema: Mwezi Februari 2017, Maria Bell alianza uhusiano na mwanachama mmoja wa genge la kigaidi la Tahrir al Sham na alituma maelfu ya jumbe za code maalumu kwa genge hilo la kigaidi.

Maafisa wa mahakama nchini Marekani wanasema kuwa, mwanajeshi huyo wa Marekani ametuma fedha mara zisizopungua 18 za thamani ya dola elfu tatu na 150 kwa waungaji mkono wa genge hilo la kigaidi katika nchi za Syria na Uturuki.

Mashtaka ya kuficha tu taarifa za fedha za magaidi yanaweza kumpelekea mwanamke huyo kufungwa miaka 10 jela kulingana na sheria za Marekani.

Wanajeshi vamizi wa Marekani nchini Syria

 

Mgogoro wa Syria ulianzishwa na maadui wa taifa hilo la Kiarabu mwaka 2011 baada ya maadui hao kumimina maelfu kwa maelfu ya magaidi ndani ya ardhi ya Syria kutoka kila kona ya Dunia. Waliokuwa mstari wa mbele katika jinai hizo ni nchi za Kiarabu hasa Saudi Arabia pamoja na Marekani, utawala wa Kizayuni na nchi jirani na Syria hasa Uturuki. 

Hata hivyo wananchi wa Syria kwa kushirikiana vilivyo na serikali yao na marafiki wa taifa hilo la Kiarabu na Kiislamu, wamefanikiwa kuwafurusha magaidi wote hao kiasi kwamba sasa hivi, mkoa wa Idlib wenye takriban watu milioni 3, ndiyo sehemu pekee waliyojikusanya magaidi na wapinzani wa serikali ya Syria wenye silaha.

Tags