Mbunge wa Bunge la Ulaya akosoa siasa za vikwazo za Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/world-i67610-mbunge_wa_bunge_la_ulaya_akosoa_siasa_za_vikwazo_za_marekani
Mbunge mmoja wa Bunge la Ulaya raia wa Ireland amekosa siasa za vikwazo za Marekani dhidi ya mataifa mengine huru yanayojitawala na kuzitaja siasa hizo kuwa ni ugaidi wa kiuchumi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 07, 2021 04:41 UTC
  • Mbunge wa Bunge la Ulaya akosoa siasa za vikwazo za Marekani

Mbunge mmoja wa Bunge la Ulaya raia wa Ireland amekosa siasa za vikwazo za Marekani dhidi ya mataifa mengine huru yanayojitawala na kuzitaja siasa hizo kuwa ni ugaidi wa kiuchumi.

Akiandika jana Jumamosii kuhusu jambo hilo katika ukurasa wake wa Twitter, Mick Wallace amesema kwamba kufikia sasa Marekani imeziwekea vikwazo nchi 38 jambo ambalo ni thibitisho la wazi la ugaidi wa kiuchumi dhidi ya nchi hizo.

Amesema jambo la kusikitisha ni kuwa katika sehemu nyingi nchi za Ulaya zimeshirikiana na Marekani katika utekelezaji wa vikwazo hivyo vya kidhalimu dhidi ya nchi hizo.

 

Mbunge huyo ameashiria nchi ya Cuba na kusema kuwa licha ya kuwa imewekewa vikwazo hivyo vya kidhalimu na Marekani lakini nchi hiyo ya Amerika ya Latini imetuma madaktari wake katika nchi 39 za dunia kwa ajili ya kupambana na virusi vya corona.

Mick Wallace amesema, dunia imekuwa ikishuhudia kuongezeka kwa siasa za upande mmoja na za mabavu za madola makubwa kupitia vikwazo vinavyotekelezwa nje ya maazimio ya Baraza la Usalama, na kuongeza kuwa inasikitisha kuona kuwa, vikwazo hivyo ambavyo kimsingi vimekuwa vikitekelezwa na Marekani, sasa vimeanza kuigwa na kutekeleza pia na Umoja wa Ulaya.

Aidha amesisitiza kuwa jambo hilo linakiuka moja kwa moja sheria za kimataifa.